Tumsifu Yesu Kristo. Karibu Katika Masomo ya Misa 22/09/2024
2024 SEPTEMBA 22: DOMINIKA YA 25 YA MWAKA
Rangi: KIJANI
Zaburi: Juma I
SOMO 1. Hek 2:12, 17-20
Zaidi ya hayo tumwotee mtu wa haki, maana hatuna haja naye, naye yu kinyume cha matendo yetu, atukaripia ya kama tumeiasi torati, na kutushitaki ya kama tumekosa adabu. Haya na tuone kama maneno yake ni kweli; tufanye kujaribu yatakayompata wakati wa mwisho wake; mradi mwenye haki akiwa ni mwana wa Mungu, Yeye atamtegemeza na kumwokoa mikononi mwa adui zake. Na tumhakikishe kwa jeuri na maumivu, ili tujifunze upole wake na kuithibitisha saburi yake akidhulumiwa. Hata tumhukumu auawe mauti ya aibu, maana ataangaliwa sawasawa na maneno yake. |
WIMBO WA KATIKATI. Zab 54: 3-8
1. Ee Mungu, kwa jina lako uniokoe, (K) Bwana ndiye anayeitegemeza nafsi yangu. 2. Kwa maana wageni wamenishambulia, 3. Tazama, Mungu anayenisaidia; |
SOMO 2. Yak 3:16-4: 3
Hapo palipo wivu na ugomvi, ndipo palipo machafuko, na kila tendo baya. Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina, haina unafiki, Na tunda la haki hupandwa katika amani na wale wafanyao amani. Vita vyatoka wapi, na mapigano yaliyoko kati yenu yatoka wapi? Si humu, katika tamaa zenu zifanyazo vita katika viungo vyenu? Mwatamani, wala hamna kitu, mwaua na kuona wivu, wala hamwezi kupata. Mwafanya vita na kupigana, wala hamna kitu kwa kuwa hamwombi! Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu. |
INJILI. Mk 9:30-37
Walitoka huko, wakapita katikati ya Galilaya; Yesu hakutaka mtu kujua. Kwa sababu alikuwa akiwafundisha wanafunzi wake, akawaambia, Mwana wa Adamu yuaenda kutiwa katika mikono ya watu, nao watamwua; hata akiisha kuuawa, baada ya siku tatu atafufuka. Lakini hawakulifahamu neno lile, wakaogopa kumwuliza. Wakafika Kapernaumu; hata alipokuwamo nyumbani, akawauliza, Mlishindania nini njiani? Wakanyamaza; kwa maana njiani walikuwa wakibishana wao kwa wao, ni nani aliye mkubwa. Akaketi chini, akawaita wale Thenashara akawaambia, Mtu atakayekuwa wa kwanza atakuwa wa mwisho kuliko wote, na mtumishi wa wote. Akatwaa kitoto, akamweka katikati yao, akamkumbatia, akawaambia, Mtu akimpokea mtoto mmoja wa namna hii kwa jina langu, anipokea mimi, na mtu akinipokea mimi, humpokea si mimi, bali yeye aliyenituma. |
TAFAKARI
UKUU KATIKA UNYENYEKEVU WA KRISTO SALA: Ee Bwana utujalie tutambue kwamba cheo ni dhamana na ukubwa ni utumishi. |