Tumsifu Yesu Kristo. Karibu Katika Masomo ya Misa 29/09/2024
2024 SEPTEMBA 29: DOMINIKA YA 26 YA MWAKA
Rangi: Kijani
Zaburi: Juma II
SOMO 1. Hes 11: 25-29
Bwana alishuka ndani ya wingu, akanena naye, akatwaa sehemu ya roho iliyokuwa juu ya Musa, akaitia juu ya wale wazee sabini; ikawa, roho hiyo ilipowashukia, wakatabiri, lakini hawakufanya hivyo tena. Lakini watu wawili walisalia kambini, jina la mmoja aliitwa Eldadi, na jina la wapili aliitwa Medadi; na roho ile ikawashukia; nao walikuwa miongoni mwao walioandikwa, lakini walikuwa hawakutoka kwenda Hemani; nao wakatabiri kambini. Mtu mmoja kijana akapiga mbio, akaenda akamwambia Musa, akasema, Eldadi na Medadi wanatoa unabii kambini. Yoshua mwana wa Nuni, mtumishi wa Musa tangu ujana wake, akajibu akasema, Ee Bwana wangu Musa, uwakataze. Musa akamwambia, Je! umekuwa na wivu kwa ajili yangu; ingekuwa heri kama watu wote wa Bwana wangekuwa manabii, na kama Bwana angewatia roho yake. |
WIMBO WA KATIKATI. Zab 19: 8, 10, 12-13, 14
1. Sheria ya Bwana ni kamilifu, (K) Maagizo ya Bwana ni ya adili, huufurahisha moyo 2. Kicho cha Bwana ni kitakatifu 3. Tena mtumishi wako huonywa kwazo, 4. Umzuie mtumishi wako asitende mambo ya kiburi, |
SOMO 2. Yak 5: 1- 6
Haya basi, enyi matajiri! Lieni, mkapige yowe kwa sababu ya mashaka yenu yanayowajia. Mali zenu zimeoza, na mavazi yenu yameliwa na nondo. Dhahabu yenu na fedha yenu zimeingia kutu, na kutu yake itawashuhudia, nayo itakula miili yenu kama moto. Mmejiwekea akiba katika siku za mwisho. Angalieni, ujira wa wakulima waliovuna mashamba yenu, ninyi mliouzuia kwa hila, unapiga kelele, na vilio vyao waliovuna vimeingia masikioni mwa Bwana wa majeshi. Mmefanya anasa katika dunia, na kujifurahisha kwa tamaa; mmejilisha mioyo yenu kama siku ya machinjo. Mmehukumu mwenye haki mkamwua; wala hashindani nanyi. |
INJILI. Mk 9: 38-43, 45, 47-48
Yohane alimwambia Yesu, Mwalimu tulimwona mtu akitoa pepo kwa jina lako, ambaye hafuatani nasi; tukamkataza, kwa sababu hafuatani nasi. Yesu akasema, Msimkataze, kwa kuwa hakuna mtu atakayefanya mwujiza kwa jina langu akaweza mara kuninenea mabaya; kwa sababu asiye kinyume chetu, yu upande wetu. Kwa kuwa ye yote atakayewanywesha ninyi kikombe cha maji, kwa kuwa ninyi ni watu wa Kristo, amin, nawaambia, hatakosa thawabu yake. Na ye yote atakayemkosesha mmojawapo wa wadogo hawa waniaminio, afadhali afungiwe jiwe la kusagia shingoni mwake, na kutupwa baharini. Na mkono wako ukikukosesha, ukate; ni afadhali kuingia katika uzima u kigutu, kuliko kuwa na mikono miwili, na kwenda zako jehanamu, kwenye moto usiozimika. Na mguu wako ukikukosesha, ukate, ni afadhali kuingia katika uzima, u kiwete, kuliko kuwa na miguu miwili, na kutupwa katika jehanum. Na jicho lako likikukosesha, ling’oe, ulitupe, ni afadhali kuingia katika ufalme wa Mungu, una chongo, kuliko kuwa na macho mawili, na kutupwa katika jehanum; ambamo humu funza wao hafi, wala moto hauzimiki. |
TAFAKARI
WEMA WA MUNGU NI KWA AJILI YA BINADAMU WOTE SALA: Ee Bwana utupe ujasiri wa kuving’oa vilema vyetu vya kiroho ili tuweze kukutumikia wewe kiaminifu. |