Masomo ya misa

Masomo ya Misa Oktoba 23

By

on

Tumsifu Yesu Kristo. Karibu Katika Masomo ya Misa 23/10/2024

2024 OKTOBA 23: JUMATANO: JUMA LA 29 LA MWAKA

Mt. Yohane wa Kapestrano, Padre
Rangi: Kijani

Zaburi: Juma I

SOMO 1. Efe 3:2-12

Mmesikia habari ya uwakili wa neema ya Mungu niliyopewa kwa ajili yenu; ya kwamba kwa kufunuliwa nalijulishwa siri hiyo, kama nilivyotangulia kuandika kwa maneno machache. Kwa hayo, myasomapo, mtaweza kuutambua ufahamu wangu katika siri yake Kristo. Siri hiyo hawakujulishwa wanadamu katika vizazi vingine; kama walivyofunuliwa mitume wake watakatifu na manabii zamani hizi katika Roho; ya kwamba Mataifa ni warithi pamoja nasi wa urithi mmoja, na wa mwili mmoja, na washiriki pamoja nasi wa ahadi yake iliyo katika Kristo Yesu kwa njia ya Injili; Injili hiyo ambayo nalifanywa mhudumu wake, kwa kadiri ya kipawa cha neema ya Mungu niliyopewa kwa kadiri ya utendaji wa uweza wake. Mimi, niliye mdogo kuliko yeye aliye mdogo wa watakatifu wote, nalipewa neema hii ya kuwahubiri Mataifa utajiri wake Kristo usiopimika; na kuwaangaza watu wote wajue habari za madaraka ya siri hiyo, ambayo tangu zamani zote ilisitirika katika Mungu aliyeviumba vitu vyote; ili sasa, kwa njia ya kanisa, hekima ya Mungu iliyo ya namna nyingi ijulikane na falme na mamlaka katika ulimwengu wa roho; kwa kadiri ya kusudi la milele alilolikusudia katika Kristo Yesu Bwana wetu. Katika yeye tunao ujasiri na uwezo wa kukaribia katika tumaini kwa njia ya kumwamini.

WOMBO WA KATIKATI. Isa 12:2-6

1. Tazama, Mungu ndiye wokovu wangu;
Nitatumaini wala sitaogopa;
Maana Bwana Yehova ni nguvu zangu
Na wimbo wangu;
Naye amekuwa wokovu wangu.
Basi, kwa furaha mtateka maji
Katika visima vya wokovu.

(K) “Kwa furaha mtateka maji
katika visima vya wokovu.

2. Mshukuruni Bwana, liitieni jina lake;
Yatangazeni matendo yake kati ya mataifa,
Litajeni jina lake kuwa kuwa limetukuka.
Mwimbieni Bwana. (K)

3. Kwa kuwa ametenda makuu,
Na yajulikane haya katika dunia yote.
Paza sauti, piga kelele, mwenyeji wa Sayuni;
Maana Mtakatifu wa Israeli ni mkuu kati yako. (K)

INJILI. Lk 12:39-48

Yesu aliwaambia wanafunzi wake: “Fahamuni neno hili, Kwamba mwenye nyumba angalijua saa atakayokuja mwivi; angalikesha, wala asingaliacha nyumba yake kuvunjwa. Nanyi jiwekeni tayari, kwa kuwa saa msiyodhani ndipo ajapo Mwana wa Adamu.” Petro akamwambia, “Bwana, mithali hiyo umetuambia sisi tu, au watu wote pia?” Bwana akasema, “Ni nani, basi, aliye wakili mwaminifu, mwenye busara, ambaye bwana wake atamweka juu ya utumishi wake wote, awape watu posho kwa wakati wake? Heri mtumwa yule, ambaye bwana wake ajapo atamkuta anafanya hivyo. Kweli nawaambia, atamweka juu ya vitu vyake vyote. Lakini, mtumwa yule akisema moyoni mwake, ‘Bwana wangu anakawia kuja,’ akaanza kuwapiga wajoli wake, wanaume kwa wanawake, akila na kunywa na kulewa; bwana wake mtumwa huyo atakuja siku asiyodhani na saa asiyojua, atamkata vipande viwili, na kumwekea fungu lake pamoja na wasioamini. Na mtumwa yule aliyejua mapenzi ya bwana wake, asijiweke tayari, wala kuyatenda mapenzi yake, atapigwa sana. Na yule asiyejua, naye amefanya yastahiliyo mapigo, atapigwa kidogo. Na kila aliyepewa vingi, kwake huyo vitatakwa vingi; naye waliyemwekea amana vitu vingi, kwake huyo watataka na zaidi.

TAFAKARI

Uwajibikaji na zawadi ya Mbinguni: Ingawa watu wengi wanapata au kuonja zawadi katika maisha haya kwa sababu ya utii wao kwa Mungu, hili haliko hivi wakati wote. Kama ingekuwa hivyo tungeingia katika kishawishi cha kujisifia mafanikio yetu na kwamba kwa kutenda mema, tumepata haya tuliyopata. Yesu anasema, kama tunataka zawadi sasa, hatutapata nyingine baadaye. Zawadi ya mbinguni ambayo wataipata wakristo ndiyo iliyo sahihi kabisa kwa yale waliyofanya hapa duniani, na zawadi hiyo itakuwa kubwa kuliko wanavyoweza kufikiri. Kwa hiyo tumtumikie Mungu kwa uaminifu katika wajibu ule aliotupatia. Yesu amewaonesha wafuasi wake jinsi wanavyopaswa kuishi hata atakapokuja. Tunapaswa kukesha, kufanya kazi kwa bidii, na kutii amri zake. Tabia hiyo ni muhimu sana hasa kwa wale ambao ni viongozi. Kiongozi mwaminifu atapatiwa fursa na wajibu mwingi zaidi. Kadiri ya wajibu na vipawa alivyonyavyo kiongozi ndivyo anavyotakiwa kuwajibika na kutumia ipasavyo. Tuwajibike kwa kutumia vyema vipaji alivyotujalia Mungu.

SALA: Mungu Mwenyezi utujalie tuwe waaminifu katika wajibu ule uliotujalie ili siku moja tuweze kupata tuzo.

The post Masomo ya Misa Oktoba 23 appeared first on CLARETIAN PUBLICATIONS-EAST AFRICA.

About mzigotv

Nyimbo Mpya 2025 2024 2023 2022 Download Audio, Video, Mp3, Mp3 African music, Tanzania Music, Naijamusic, naijavibe, Bekaboy, Djmwanga, Tanzania songs, Kenya songs, Uganda songs, Rwanda songs, Congo songs, Zanzibar, Singeli, Taarabu, Reggae, Amapiano, Nyimbo za dini, Gospel songs, Diamond platnumz, jux, Rayvanny, Harmonize, Nandy, Zuchu, Wasafi, Alikiba Teading songs, Top 100 songs youtube, Nigeria, Naija songs.

Recommended for you