Tumsifu Yesu Kristo. Karibu Katika Masomo ya Misa 08/10/2024
2024 OKTOBA 8: JUMANNE-JUMA LA 27 LA MWAKA
Mt. Reparata
Rangi:Kijani
Zaburi: Juma III
SOMO 1. Gal 1:13-24
Mmesikia habari za mwenendo wangu zamani katika dini ya Kiyahudi, kwamba naliliudhi kanisa la Mungu kupita kiasi, nikaliharibu. Nami naliendelea katika dini ya Kiyahudi kuliko wengi walio hirimu zangu katika kabila yangu, nikajitahidi sana katika kuyashika mapokeo ya baba zangu. Lakini Mungu, aliyenitenga tangu tumboni mwa mama yangu, akaniita kwa neema yake, alipoona vema kumdhihirisha Mwanawe ndani yangu, ili niwahubiri Mataifa habari zake; mara sikufanya shauri na watu wenye mwili na damu; wala sikupanda kwenda Yerusalemu kwa hao waliokuwa mitume kabla yangu; bali nalikwenda zangu Arabuni, kisha nikarudi tena Dameski. Kisha, baada ya miaka mitatu, nalipanda kwenda Yerusalemu ili nionane na Kefa, nikakaa kwake siku kumi na tano. Lakini sikumwona mtume mwingine, ila Yakobo, ndugu yake Bwana. Na hayo ninayowaandikia, angalieni, mbele za Mungu, sisemi uongo. Baadaye nalikwenda pande za Shamu na Kilikia. Lakini sikujulikana uso wangu na makanisa ya Uyahudi yaliyokuwa katika Kristo; ila wamesikia tu ya kwamba huyo aliyetuudhi hapo kwanza, sasa anaihubiri imani ile aliyoiharibu zamani. Wakamtukuza Mungu kwa ajili yangu. |
WIMBO WA KATIKATI. Zab 139:1-3, 13-15
1. Ee Bwana umenichunguza na kunijua. (K) Uniongoze, Ee Bwana, katika njia ya milele. 2. Maana Wewe ndiwe uliyeniumba mtima wangu, 3. Na nafsi yangu yajua sana, |
INJILI. Lk 10:38-42
Yesu aliingia katika kijiji kimoja; mwanamke mmoja jina lake Martha akamkaribisha nyumbani kwake. Naye alikuwa na umbu lake aitwaye Mariamu, aliyeketi miguuni pake Yesu, akasikiliza maneno yake. Lakini Martha alikuwa akihangaika kwa utumishi mwingi; akamwendea, akasema, “Bwana, huoni vibaya hivyo ndugu yangu alivyoniacha nitumike peke yangu? Basi mwambie anisaidie.” Bwana akajibu akamwambia, “Martha, Martha, unasumbuka na kufadhaika kwa ajili ya vitu vingi; lakini kinatakiwa kitu kimoja tu; na Mariamu amelichagua fungu lililo jema, ambalo hataondolewa.” |
TAFAKARI.
WAFANYAKAZI TUWE MAKINI: Wale tunaofanya kazi kwa bidii tunapaswa kuwa makini. Yapo matatizo makubwa matatu yanaweza kututokea: Mosi; unapoomba msaada (msaada halali) usilenge katika kuonesha mafanikio yako mwenyewe au kujigamba (Unakwenda kuomba msaada huku unajisifia). “Bwana, huoni vibaya hivyo ndugu yangu alivyoniacha nitumike peke yangu? Pili; Unapomwita Yesu “Bwana” huku unahoji maamuzi na mamlaka yake au kumuonesha kwamba haongozi timu yake sawa sawa, unamuonesha Yesu kwamba wewe ni bora zaidi kuliko Yeye. Tatu; Unapokubali uhusiano wako na mtu mwingine, kama Martha alivyofanya kwa dada yake, kisha unampinga kwa kushindwa kufuata maongozi yako, unayafanya matakwa yako kuwa sahihi na bora zaidi kuliko yake hii ni kwa sababu pengine zina matokeo mazuri. Lakini njia iliyo bora ni hii; Usijitafutie au kujitangazia ukuu wako mwenyewe. Wasaidie wengine katika wajibu wao muhimu. Muombe Yesu kwanza kisha nenda kafanye kazi yako halali. SALA: Bwana utusaidie tuwe wanyenyekevu tusijitafutie ukuu wala kuwadharau wengine ikiwa sisi tunafanya vyema zaidi. |