Mzigo-TV-728x90

Masomo ya misa

Masomo ya Misa Novemba 2

By

on

Tumsifu Yesu Kristo. Karibu Katika Masomo ya Misa 02/11/2024

2024 NOVEMBA 2: JUMAMOSI: JUMA LA 30 LA MWAKA

KUMBUKUMBU YA WAAMINI MAREHEMU WOTE
Rangi: Nyeupe

Zaburi: Tazama sala ya siku

SOMO 1. Hek 3: 1-9

Roho zao wenye haki wamo mkononi mwa Mungu, wala maumivu hayatawagusa. Machoni pa watu walio wajinga walionekana kwamba wamekufa, na kufariki kwao kulidhaniwa kuwa ni hasara yao, na kusafiri kwao kutoka kwetu kuwa ni uharibifu wao; bali wao wenyewe wamo katika amani. Kwa sababu hata ikiwa (waonavyo watu) wanaadhibiwa, hata hivyo taraja lao limejaa kutokufa, na wakiisha kustahimili kurudiwa kidogo watapokea wingi wa mema. Kwa kuwa Mungu amewajaribu, na kuwaona kuwa wamemstahili, kama dhahabu katika tanuru aliwajaribu, akawakubali mithili ya kafara. Wakati wa kujiliwa kwao watang’aa, na kama vimulimuli katika mabua makavu watametameta. Watahukumu mataifa na kuwatawala kabila za watu; naye Bwana atawamiliki milele na milele. Wenye kumtumaini watafahamu yaliyo kweli, na waaminifu watakaa naye katika upendo; mradi neema na rehema zina wateule wake.

WIMBO WA KATIKATI. Zab 23

1. Bwana ndiye mchungaji wangu,
Sitapungukiwa na kitu.
Katika malisho ya majani mabichi hunilaza,
Kando ya maji ya utulivu huniongoza.

(K) Bwana ndiye mchungaji wangu sitapungukiwa na kitu.

2. Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongoza
Katika njia za haki kwa ajili ya jina lake.
Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti,
Sitaogopa mabaya;
Kwa maana Wewe upo pamoja nami,
Gongo lako na fimbo yako vyanifariji. (K)

3. Waandaa meza mbele yangu,
Machoni pa watesi wangu,
Umenipaka mafuta kichwani pangu,
Na kikombe changu kinafurika.(K)

4. Hakika wema na fadhili zinznifuata,
Siku zote za maisha yangu,
Nami nitakaa nyumbani mwa Bwana milele. (K)

SOMO 2. Rum 6: 3-9

Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake? Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima. Kwa maana kama tulivyounganika naye katika mfano wa mauti yake, kadhalika tutaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake; tukijua neno hili, ya kuwa utu wetu wa kale ulisulibishwa pamoja naye, ili mwili wa dhambi ubatilike, tusitumikie dhambi tena; kwa kuwa yeye aliyekufa amehesabiwa haki mbali na dhambi. Lakini tukiwa tulikufa pamoja na Kristo, twaamini ya kuwa tutaishi pamoja naye; tukijua ya kuwa Kristo akiisha kufufuka katika wafu hafi tena, wala mauti haimtawali tena.

INJILI. Mt 25: 31-46

Yesu aliwaambia Wanafunzi wake: Hapo atakapokuja mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake; na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi; atawaweka kondoo mkono wake wa kuume, na mbuzi mkono wake wa kushoto.  Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme, mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu; kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha; nalikuwa uchi, mkanivika; nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijia. Ndipo wenye haki watakapomjibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona una njaa, tukakulisha, au una kiu tukakunywesha? Tena ni lini tulipokuona u mgeni, tukakukaribisha, au u uchi, tukakuvika? Ni lini tena tulipokuona u mgonjwa, au kifungoni, tukakujia? Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amini, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi. Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake; kwa maana nalikuwa na njaa, msinipe chakula; nalikuwa na kiu, msininyweshe; nalikuwa mgeni, msinikaribishe; nalikuwa uchi, msinivike; nalikuwa mgonjwa, na kifungoni, msije kunitazama. Ndipo hao pia watajibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona wewe una njaa, au una kiu, au u mgeni au u uchi, au u mgonjwa, au u kifungoni, tusikuhudumie? Naye atawajibu, akisema, Amini, nawaambia, Kadiri msivyomtendea mmojawapo wa hao walio wadogo, hamkunitendea mimi.  Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele.

TAFAKARI

MUNGU NI MKARIMU: Inaonekana Mungu anataka kuwa mkarimu hata katika siku ile ya hukumu. Tutazawadiwa kwa mema ambayo tumeyafanya hata kama hutukujua kwamba tumeyafanya, au hukujua kwamba Yesu alikuwa anatutazama. Jambo hilo litufanye tuendeleze mtindo wa maisha ya upendo kusudi matendo mema yatiririke kutoka katika maisha yetu ya kawaida. Kwa kuwa Mungu ni mkarimu nasi tunapaswa kuwa wakarimu, Mungu ni mvumilivu nasi tuwe wavumilivu, tunapaswa kujifunza kuishi hivyo. Baadhi ya mambo ambayo unayapuuzia na kuyaona kuwa ya kawaida kabisa, kwa Mungu yanaweza kuwa ni ya thamani sana. Kuwa mwema katika mambo ya kawaida kabisa ya kila siku kama kumpatia mtu maji ya kunywa. Mambo madogo tunayofanya yanakuwa mambo makubwa. Mungu ayabadili maisha yako ya ubinafsi yawe ya ukarimu na huruma. Mungu ni mkuu sana msadiki. Huo ni ujumbe unaoupata kila mara unapofanya matendo fulani yanayoonesha upendo kwa Mungu na kwa jirani.

SALA: Ee Mungu utufanye tuwe wakarimu na wema kwa wahitaji pasipo ubaguzi wowote.

The post Masomo ya Misa Novemba 2 appeared first on CLARETIAN PUBLICATIONS-EAST AFRICA.

About mzigotv

Nyimbo Mpya 2023, 2022 Download Audio, Video, Mp3, Mp3 African music, Tanzania Music, Naijamusic, naijavibe, Bekaboy, Djmwanga, Tanzania songs, Kenya songs, Uganda songs, Rwanda songs, Congo songs, Zanzibar, Singeli, Taarabu, Reggae, Amapiano, Nyimbo za dini, Gospel songs, Diamond platnumz, jux, Rayvanny, Harmonize, Nandy, Zuchu, Wasafi, Alikiba Teading songs, Top 100 songs youtube, Nigeria, Naija songs.

Recommended for you