Mzigo-TV-728x90

Masomo ya misa

Masomo ya Misa Agosti 7

By

on

Tumsifu Yesu Kristo. Karibu Katika Masomo ya Misa 07/08/2024

2024 AGOSTI 7: -JUMA LA 18 LA MWAKA

Mt Sisto II, Papa na wenzake Mashahidi
Rangi: Kijani

Zaburi: Juma 2

Somo 1. Yer 31:1-7

“Wakati huo, asema Bwana, nitakuwa Mungu wa jamaa zote za Israeli, nao watakuwa watu wangu.” Bwana asema hivi, “Watu wale walioachwa na upanga walipata neema jangwani; yaani, Israeli, hapo nilipokwenda kumstarehesha.” Bwana alinitokea zamani, akisema, “Naam, nimekupenda kwa upendo wa milele, ndiyo maana nimekuvuta kwa fadhili zangu. Mara ya pili nitakujenga, nawe utajengwa, Ee bikira wa Israeli, mara ya pili utapambwa kwa matari yako, nawe utatokea katika michezo yao wanaofurahi. Mara ya pili utapanda mizabibu juu ya milima ya Samaria; wapanzi watapanda, nao watayafurahia matunda yake. Maana kutakuwa siku moja, ambayo walinzi watalia juu ya vilima vya Efraimu, ‘Inukeni, tukaende Sayuni, kwa Bwana, Mungu wetu.’” Maana Bwana asema hivi, mwimbieni Yakobo kwa furaha, mkampigie kelele mkuu wa mataifa, tangazeni, sifuni, mkaseme, Ee Bwana, uwaokoe watu wako mabaki ya Israeli.

Wimbo wa Katikati. Yer 31:10-131

1. Lisikieni neno la Bwana,
enyi mataifa, litangazeni visiwani mbali,
mkaseme, Aliyemtawanya Israeli atamkusnya,
na kumlinda, kama mchungaji alindavyo kundi lake.
Kwa maana Bwana amemweka huru Yakobo,
amemkomboa mkononi mwake
aliyekuwa hodari kuliko yeye.

(K) Bwana atatulinda kama mchungaji alindavyo kundi lake.

2. Nao watakuja, na kuimba katika mlima Sayuni,
wataukimbilia wema wa Bwana, nafaka, na divai;
na mafuta, na wachanga wa kondoo na wa ng’ombe;
na roho zao zitakuwa kama bustani iliyotiwa maji;
wala hawatauzunika tena kabisa. (K)

3. Ndipo bikira atafurahi katika kucheza,
na vijana na wazee pamoja;
maana nitageuza masikitiko yao kuwa furaha,
nami nitawafariji,
na kuwafurahisha waache huzuni zao. (K)

Injili. Mt 15:21-28

Yesu aliondoka Genezareti akaenda kando pande za Tiro na Sidoni. Na tazama, mwanamke Mkananayo wa mipaka ile akatokea, akampazia sauti akisema, “Unirehemu, Bwana, Mwana wa Daudi; binti yangu amepagawa sana na pepo.”  Wala yeye hakumjibu neno. Nao wanafunzi wake wakamwendea, wakamwomba, wakisema, “Mwache aende zake; kwa maana anapiga kelele nyuma yetu.” Akajibu, akasema, “Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.”  Naye akaja akamsujudia, akisema, “Bwana unisaidie. Akajibu, akasema, Si vema kukitwaa chakula cha wototo na kuwatupia mbwa.” Akasema, “Ndiyo, Bwana, lakini hata mbwa hula makombo yaangukayo mezani pa bwana zao.” Ndipo Yesu akajibu, akamwambia, “Mama, imani yako ni kubwa; na iwe kwako kama utakavyo.” Akapona binti yake tangu saa ile.

TAFAKARI

UPENDO WA MUNGU NI WA MILELE, UNATUFANYA WAPYA: Unabii wa Yeremia katika somo la leo, ni mwaliko wa kutambua na kulipokea pendo la Mungu. Tunapokosa mahusiano mema na Mungu tukaenda mbali na pendo lake, maisha huwa ya shida na taabu, kwani hatuna ulinzi wa uhakika. Leo, tunaalikwa kama Israeli mteule wa Mungu kupokea unabii huo uliojaa upendo, ili tukajengeke upya, tuwe wapya katika imani, mahusiano, na hata shughuli tulizoshindwa kukamilisha kutokana na mafarakano zikamalizike kwa Baraka za Mungu ili nasi tuweze kusema, “Bwana uwaokoe watu wako.” Injili inaweka mbele yetu nguvu ya pendo la Mungu linalofanya yote kuwa mapya. Kupokea ukamilifu wa pendo la Mungu imani thabiti inatakiwa. Sisi nasi tunayo mahitaji ya kumwambia Yesu. Ni kwa njia imani twaweza kustahilishwa maombi yetu. Tuzingatie anachosema Yesu: Imani yako ni kubwa; na iwe kwako kama utakavyo.”

SALA: Ee Bwana utujalie paji la imani.

About mzigotv

Nyimbo Mpya 2023, 2022 Download Audio, Video, Mp3, Mp3 African music, Tanzania Music, Naijamusic, naijavibe, Bekaboy, Djmwanga, Tanzania songs, Kenya songs, Uganda songs, Rwanda songs, Congo songs, Zanzibar, Singeli, Taarabu, Reggae, Amapiano, Nyimbo za dini, Gospel songs, Diamond platnumz, jux, Rayvanny, Harmonize, Nandy, Zuchu, Wasafi, Alikiba Teading songs, Top 100 songs youtube, Nigeria, Naija songs.

Recommended for you