Tumsifu Yesu Kristo. Karibu Katika Masomo ya Misa 18/08/2024
2024 AGOSTI 18: DOMINIKA YA 20 YA MWAKA
Rangi: Kijani
Zaburi: Juma IV
Somo 1. Mit 9: 1-6
Hekima ameijenga nyumba yake, Amezichonga nguzo zake saba; Amechinja nyama zake, amechanganya divai yake, Ameiandalia meza yake pia. Amewatuma wajakazi wake, analia, Mahali pa mjini palipoinuka sana, Kila aliye mjinga na aingie humu, Tena amwambia mtu aliyepungukiwa na akili, Njoo ule mkate wangu, Ukanywe divai niliyoichanganya. Enyi wajinga, acheni ujinga, mkaishi, Mkaende katika njia ya ufahamu. |
Wimbo wa Katikati. ” Zab 34: 2-3, 10-15″
1. Nitamhimidi Bwana kila wakati, (K) Onjeni mwone ya kuwa Bwana yu mwema. 2. Mcheni Bwana, enyi watakatifu wake, 3. Njoni, enyi wana, mnisikilize, 4. Uuzuie ulimi wako na mabaya, |
Somo 2. Efe 5: 15-20
Angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima, bali kama watu wenye hekima; mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu. Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana. Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho; mkisemezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu; na kumshukuru Mungu Baba siku zote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo. |
Injili. Yn 6: 51-59
Yesu aliwaambia makutano: Mimi ndimi chakula chenye uzima kilichoshuka kutoka mbinguni; mtu akila chakula hiki, ataishi milele. Na chakula nitakachotoa mimi ni mwili wangu, kwa ajili ya uzima wa ulimwengu. Basi Wayahudi walishindana wao kwa wao wakisema, Awezaje mtu huyu kutupa sisi mwili wake ili tuule? Basi Yesu akawaambia, Amin, amin nawaambieni, Msipoula mwili wake Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu. Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa milele, nami nitamfufua siku ya mwisho. Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli, na damu yangu ni kinywaji cha kweli. Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami hukaa ndani yake. Kama vile baba aliye hai alivyonitumia mimi, nami ni hai kwa Baba; kadhalika naye mwenye kunila atakuwa hai kwa mimi. Hiki ndicho chakula kishukacho kutoka mbinguni; si kama mababa walivyokula, wakafa; bali akilaye chakula hicho ataishi milele. Maneno hayo aliyasema katika sinagogi, alipokuwa akifundisha, huko Kapernaumu.
TAFAKARI
EKARISTI TAKATIFU INATUFANYA KUWA HAI KATIKA KRISTO SALA: Ee Yesu utujalie tuungane nawe zaidi kila tunapokula Mwili wako na kuinywa Damu yako.
|