Tumsifu Yesu Kristo. Karibu Katika Masomo ya Misa 11/08/2024
2024 AGOSTI 11: DOMINIKA YA 19 YA MWAKA
Rangi: Kijani
Zaburi: Juma III
Somo 1. 1 Fal 19: 4-8
Eliya yeye mwenyewe aliendelea katika jangwa mwendo wa siku moja, akaenda akaketi chini ya mretemu. Akajiombea roho yake afe, akasema, Yatosha sasa, Ee Bwana, uiondoe roho yangu; kwa kuwa mimi si mwema kuliko Baba zangu. Naye akajinyosha akalala chini ya mretemu; na tazama, malaika akamgusa, akamwambia, Inuka, ule. Akatazama, kumbe! pana mkate umeokwa juu ya makaa, na gudulia la maji, kichwani pake. Akala, akanywa, akajinyosha tena. Malaika wa Bwana akamwendea mara ya pili, akamgusa, akasema, Inuka, ule, maana safari hii ni kubwa mno kwako. Akainuka, akala, akanywa, akaenda katika nguvu za chakula hicho siku arobaini mchana na usiku hata akafika Horebu, mlima wa Mungu. |
Wimbo wa Katikati. Zab 34: 2-9
1. Nitamhimidi Bwana kila wakati wakati, (K) Onjeni mwone ya kuwa Bwana yu mwema. 2. Mtukuzeni Bwana pamoja nami, 3. Wakamwelekea macho wakatiwa nuru, 4. Malaika wa Bwana hufanya kituo, |
Somo 2. Efe 4: 30-5:2
Msimhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu; ambaye kwa yeye mlitiwa muhuri hata siku ya ukombozi. Uchungu wote na ghadhabu na hasira na kelele na matukano yaondoke kwenu, pamoja na kila namna ya ubaya; tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama na Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi. Hivyo mfuateni Mungu, kama watoto wanaopendwa; mkaenende katika upendo, kama Kristo naye alivyowapenda ninyi; tena akajitoa kwa ajili yetu, sadaka na dhabihu kwa Mungu, kuwa harufu ya manukato. |
Injili. Yn 6: 41-51
Wayahudi walimnung’unikia Yesu kwa sababu alisema, Mimi ni chakula kilichoshuka kutoka mbinguni. Wakasema, Huyu siye Yesu, mwana wa Yusufu, ambaye twamjua babaye na mamaye? Sasa asemaje huyu, Nimeshuka kutoka Mbinguni? Basi Yesu akajibu, akawaambia, Msinung’unike ninyi kwa ninyi. Hakuna mtu awezaye kuja kwangu, asipovutwa na Baba aliyenipeleka; nami nitamfufua siku ya mwisho. Imeandikwa katika manabii, Na wote watakuwa wamefundishwa na Mungu. Basi kila aliyesikia na kujifunza kwa Baba huja kwangu. Si kwamba mtu amemuona Baba, ila yeye atokaye kwa Mungu; huyo ndiye aliyemwona Baba. Amin, amin, nawaambia, Yeye aaminiye yuna uzima wa milele. Mimi ndimi chakula cha uzima. Baba zenu waliila mana jangwani; wakafa. Hiki ni chakula kishukacho kutoka mbinguni, kwamba mtu akile wala asife. Mimi ndimi chakula chenye uzima kilichoshuka kutoka mbinguni; mtu akila chakula hiki, ataishi milele. Na chakula nitakachotoa mimi ni mwili wangu, kwa ajili ya uzima wa ulimwengu. |
TAFAKARI
UWEPO WA KRISTO KATI YETU NI HAKIKA YA KUUPATA UZIMA WA MILELE SALA: Ee Bwana Yesu utulishe kwa Mwili wako ili tupate uzima wa milele. |