Mzigo-TV-728x90

Masomo ya misa

JANUARI 10, 2024 JUMATANO. JUMA LA 1 LA MWAKA

By

on

JANUARI 10, 2024 JUMATANO. JUMA LA 1 LA MWAKA

Kijani

Zaburi. Juma 1

Mtakatifu: William wa Burse, Askofu

Utume: Aliishi kitakatifu mpole na mkunjufu na mwenyekicheko.

Usomi: Alikuwa askofu wa Burje (Ufaransa).

Kufariki : Alizikwa katika Kanisa la Burje miujiza mingi ilitendeka juu yake.

Masomo

Somo 1. 1 Sam 3:1-10, 19-20

Mtoto Samweli alimtumikia Bwana mbele ya Eli. Na neno la Bwana lilikuwa adimu siku zile; hapakuwa na mafunuo dhahiri. Ikawa wakati huo, Eli alipokuwa amelala mahali pake tena macho yake yalikuwa yameanza kupofuka, hata asiweze kuona, na taa ya Mungu ilikuwa haijazimika bado, na Samweli alikuwa amelala katika hekalu la Bwana, palipokuwa na sanduku la Mungu; basi, wakati huo Bwana akamwita Samweli; naye akasema, “Mimi hapa.” Akamwendea Eli kwa haraka, akasema, “Mimi hapa; kwa maana uliniita.” Akasema, Sikukuita; kalale tena. Naye akaenda, akalala tena. Bwana akaita mara ya pili, “Samweli! Samweli!” Akaondoka akamwendea Eli, akasema, “Mimi hapa; kwa maana uliniita.” Akajibu, “Sikukuita, mwanangu; kalale tena.” Basi Samweli alikuwa hamjui Bwana bado, na neno la Bwana lilikuwa bado halijafunuliwa kwake. Bwana akamwita Samweli mara ya tatu. Naye akaondoka akamwendea Eli, akasema, “Mimi hapa; kwa maana uliniita.” Ndipo Eli akatambua ya kuwa Bwana ndiye aliyemwita yule mtoto. Kwa hiyo Eli akamwambia Samweli, “Enenda, kalale; itakuwa, akikuita, utasema, Nena, Bwana; kwa kuwa mtumishi wako anasikia.” Basi Samweli akaenda akalala mahali pake. Bwana akaja, akasimama, akaita vile vile kama kwanza, “Samweli! Samweli!” Ndipo Samweli akasema, “Nena, Bwana; kwa kuwa mtumishi wako anasikia.” Samweli akakua, naye Bwana alikuwa pamoja naye, wala hakuliacha neno lake lo lote lianguke chini. Nao Waisraeli wote, toka Dani mpaka Beer-sheba, walitambua ya kwamba huyo Samweli amewekwa kuwa nabii wa Bwana.

Zaburi. 40:2, 5, 7-10

  1. Nalimngoja Bwana kwa Saburi, akaniinamia akakisikia kilio changu.
    Heri aliyemfanya Bwana kuwa tumaini lake, wala hakuwaelekea wenye kiburi
    wala hao wanaogeukia uongo. (K)

(K) Tazama nimekuja kuyafanya mapenzi yako, Ee Bwana.

  • Dhabihu na matoleo hukupendezwa nazo, Masikio yangu umeyazibua,
    Kafara na sadaka za dhambi hukuzitaka. Ndipo niliposema, Tazama nimekuja. (K)
  • Katika gombo la chuo imeandikwa, kuyafanya mapenzi yako,
    Ee Mungu wangu, ndiyo furaha yangu, Naam, sharia yako imo moyoni mwangu. (K)
  • Nimehubiri habari za haki katika kusanyiko kubwa, Sikuizuia midomo yangu, Ee Bwana, unajua. (K)

Injili. Mk 1: 29-39

Siku ile, Yesu alipotoka katika sinagogi, walifika nyumbani kwa Simoni na Andrea, pamoja na Yakobo na Yohane. Naye mkwewe Simoni, mamaye mkewe, alikuwa kitandani, hawezi homa; na mara wakamwambia habari zake. Akamkaribia, akamwinua kwa kumshika mkono, homa ikamwacha, akawatumikia. Hata kulipokuwa jioni, na jua limekwisha kuchwa, walikuwa wakimletea wote waliokuwa hawawezi, na wenye pepo. Na mji wote ulikuwa umekusanyika mlangoni. Akaponya wengi waliokuwa na maradhi mbalimbali, akatoa pepo wengi, wala hakuwaacha pepo kunena, kwa sababu walimjua. Hata alfajiri na mapema sana akaondoka, akatoka akaenda zake mahali pasipokuwa na watu, akaomba huko. Simoni na wenziwe wakamfuata; nao walipomwona wakamwambia, “Watu wote wanakutafuta.” Akawaambia, “Twendeni mahali pengine, mpaka vijiji vilivyo karibu, nipate kuhubiri huko nako; maana kwa hiyo nalitokea.” Akaenda akihubiri katika masinagogi yao, katika nchi yote ya Galilaya, na kutoa pepo.

Tafakari

TUNAITWA KUTUMIKIA: Katika utumishi wake Eli, tunashuhudia mtoto Samweli akiitwa na Bwana. Kwake ilikuwa vigumu kuitambua sauti ya Bwana na ndipo Eli akamsaidia kuitambua Sauti hiyo na hivyo Samweli anaitika wito wa Kinabii na anamtumikia Bwana. Waisraeli wanamtambua kwa sababu amekuwa akiwatumikia. Katika Injili Yesu Kristo amekuwa akiwatumikia ndugu zake, amemponya homa mkwewe Simoni, ameponya wote waliokuwa hawawezi na wenye pepo waliopelekwa kwake. Pia amekuwa akihubiri sehemu mbalimbali katika masinagogi. Wapendwa Taifa la Mungu, katika maisha yetu kila mmoja ameitwa na Mungu kuwatumikia wenzake katika nafasi yake, inaweza kuwa katika maisha ya ndoa, wito wa upadre, utawa, hata katika kazi nyingine. Katika kutumikia huku daima inatupasa kuwa tayari kujitolea bila kujali malipo, bila kuweka vikwazo au visingizio fulani. Hivyo nasi tuwe tayari kutumikia muda wote na bila kuchoka.

SALA: Ee Yesu unipe moyo wa utumishi kwako na kwa jirani. Amina.

The post JANUARI 10, 2024 JUMATANO. JUMA LA 1 LA MWAKA appeared first on Claretian Publications.

About mzigotv

Nyimbo Mpya 2023, 2022 Download Audio, Video, Mp3, Mp3 African music, Tanzania Music, Naijamusic, naijavibe, Bekaboy, Djmwanga, Tanzania songs, Kenya songs, Uganda songs, Rwanda songs, Congo songs, Zanzibar, Singeli, Taarabu, Reggae, Amapiano, Nyimbo za dini, Gospel songs, Diamond platnumz, jux, Rayvanny, Harmonize, Nandy, Zuchu, Wasafi, Alikiba Teading songs, Top 100 songs youtube, Nigeria, Naija songs.

Recommended for you