Mzigo-TV-728x90

Masomo ya misa

Masomo ya Misa Septemba 3

By

on

Tumsifu Yesu Kristo. Karibu Katika Masomo ya Misa 03/09/2024

2024 SEPTEMBA 3: JUMANNE-JUMA LA 22 LA MWAKA

Mt. Gregori Mkuu, Papa na Mwalimu wa Kanisa
Rangi: Nyeupe

Zaburi: Juma 2

Somo 1. 1 Kor 2:10-16

Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu. Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu. Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliokirimiwa na Mungu. Nayo twayanena, si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho, tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni. Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni. Lakini mtu wa rohoni huyatambua yote, wala yeye hatambuliwi na mtu. Maana, Ni nani aliyeifahamu nia ya Bwana, amwelimishe? Lakini sisi tunayo nia ya Kristo.

Wimbo wa Katikati. Zab 145:8-14

1. Bwana ana fadhili, ni mwingi wa huruma,
Si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema,
Bwana ni mwema kwa watu wote
Na rehema zake zi juu ya kazi zake zote.

(K) Bwana ni mwenye haki katika njia zake zote.

2. Ee Bwana, kazi zako zote zitakushukuru,
Na wacha Mungu wako watakuhimidi.
Wataunena utukufu wa ufalme wako,
Na kuuhadithia uweza wako.
Ili kuwajulisha watu matendo yake makuu,
Na utukufu wa fahari ya ufalme wake. (K)

3. Ufalme wako ni ufalme wa zamani zote,
Na mamlaka yako ni ya vizazi vyote.
Bwana huwategemeza wote waangukao,
Huwainua wote walioinama chini. (K)  

Injili. Lk 4:31-37

Yesu alishuka mpaka Kapernaumu, mji wa Galilaya, akawa akiwafundisha siku ya sabato; wakashangaa mno kwa mafundisho yake, kwa kuwa neno lake lilikuwa na uwezo. Na ndani ya sinagogi mlikuwa na mtu mwenye roho ya pepo mchafu, akalia kwa sauti kuu, akisema, Acha! Tuna nini nawe, Yesu wa Nazareti? Umekuja kutuangamiza? Nakujua u nani, Mtakatifu wa Mungu. Yesu akamkemea, akisema, Fumba kinywa, mtoke. Ndipo yule pepo akamwangusha katikati, akamtoka asimdhuru neno.  Mshangao ukawashika wote, wakasemezana wakisema, Ni neno gani hili, maana awaamuru pepo wachafu kwa uwezo na nguvu, nao hutoka.  Habari zake zikaenea kila mahali katika nchi ile.

TAFAKARI

NGUVU NA MAMLAKA YA KRISTO: Kukataliwa kwa Kristo huko Nazareti imekuwa ni baraka kwa watu wa Kapernaumu, anaongea na kutenda kwa mamlaka huko. Watu wa huko walishangazwa na kufurahishwa na maneno na matendo yake, “na wakastaajabu kwa mafundisho yake, kwa maana alisema kwa mamlaka (Lk 4:32).” Mamlaka yake ilidhihirika alipoingia tu kwenye sinagogi “mtu aliyekuwa na roho ya pepo mchafu, akalia kwa sauti kuu, akisema, Acha! Tuna nini nawe, Yesu wa Nazareti? Umekuja kutuangamiza? Nakujua u nani, Mtakatifu wa Mungu (Lk 4:34).” Yesu anamkemea, fumba kinywa mtoke kwa amri hiyo pepo alimtoka bila kumdhuru (Lk 4: 35).”  Kwa uelewa wa kawaida shetani anawajibika kwa uovu wa aina yeyote ile. Anapofundisha Neno la Mungu mapepo yanatetemeka, yalitambua mamlaka na uwezo wa Kristo wa kuwadhuru na kuwaamuru wamtoke waliyemkalia. Kristo aliwanyamazisha sio tu kusema bali hata kuendelea kumdhuru waliyemkalia.

SALA: Ee Bwana utujalie neema ya kutambua na kukiri mamlaka yako.

About mzigotv

Nyimbo Mpya 2023, 2022 Download Audio, Video, Mp3, Mp3 African music, Tanzania Music, Naijamusic, naijavibe, Bekaboy, Djmwanga, Tanzania songs, Kenya songs, Uganda songs, Rwanda songs, Congo songs, Zanzibar, Singeli, Taarabu, Reggae, Amapiano, Nyimbo za dini, Gospel songs, Diamond platnumz, jux, Rayvanny, Harmonize, Nandy, Zuchu, Wasafi, Alikiba Teading songs, Top 100 songs youtube, Nigeria, Naija songs.

Recommended for you