Mzigo-TV-728x90

Masomo ya misa

Masomo ya Misa Septemba 20

By

on

Tumsifu Yesu Kristo. Karibu Katika Masomo ya Misa 19/09/2024

2024 SEPTEMBA 19: ALHAMISI-JUMA LA 24 LA MWAKA

Mt. Januari, Askofu na Shahidi
Rangi: Kijani

Zaburi: Juma IV

SOMO 1. 1 Kor 15:1-11

Ndugu zangu, nawaarifu ile injili niliyowahubiri; ambayo ndiyo mliyoipokea, na katika hiyo mnasimama, na kwa hiyo mnaokolewa; ikiwa mnayashika sana maneno niliyowahubiri; isipokuwa mliamini bure. Kwa maana naliwatolea ninyi hapo mwanzo yale niliyoyapokea mimi mwenyewe, ya kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo Maandiko; na ya kuwa alizikwa;  na ya kuwa alifufuka siku ya tatu, kama yanenavyo Maandiko; na ya kuwa alimtokea Kefa; tena na wale Thenashara; baadaye aliwatokea ndugu zaidi ya mia tano pamoja; katika hao wengi wanaishi hata sasa, ila baadhi yao wamelala; baadaye akamtokea Yakobo; tena na mitume wote; na mwisho wa watu wote, alinitokea mimi, kama ni mtu aliyezaliwa si kwa wakati wake. Maana mimi ni mdogo katika mitume, nisiyestahili kuitwa mtume, kwa sababu naliliudhi Kanisa la Mungu. Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo; na neema yake iliyo kwangu ilikuwa si bure, bali nalizidi sana kufanya kazi kupita wao wote; wala si mimi, bali ni neema ya Mungu pamoja nami. Basi, kama ni mimi, kama ni wale, ndivyo tuhubirivyo, na ndivyo mlivyoamini.

WIMBO WA KATIKATI. Zab 118: 1b-2, 16a-17, 28

1. Aleluya.
Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema,
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
Israeli na aseme sasa,
Ya kwamba fadhili zake ni za milele.

(K) Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema.

2. Mkono wa kuume wa Bwana umetukuzwa;
Mkono wa kuume wa Bwana hutenda makuu.
Sitakufa bali nitaishi,
Nami nitayasimulia matendo ya Bwana. (K)

3. Ndiwe Mungu wangu, nami nitakushukuru,
Ndiwe Mungu wangu, name nitakutukuza. (K)         

INJILI. Lk 7:36-50

Mtu mmoja katika Mafarisayo alimwalika Yesu ale chakula kwake; akaingia katika nyumba yake yule Farisayo, akaketi chakulani. Na tazama, mwanamke mmoja wa mji ule, aliyekuwa mwenye dhambi, alipopata habari ya kuwa ameketi chakulani katika nyumba ya yule Farisayo, alileta chupa ya marimari yenye marhamu. Akasimama nyuma karibu na miguu yake, akilia, akaanza kumdondoshea machozi yake, na kuipangusa kwa nywele za kichwa chake, akiibusubusu miguu yake na kuipaka yale marhamu. Basi, yule Farisayo aliyemwalika alipoona vile, alisema moyoni mwake, “Mtu huyu kama angekuwa nabii, angemtambua mwanamke huyu amgusaye, ni nani, naye ni wa namna gani, ya kwamba ni mwenye dhambi.” Yesu akajibu akamwambia, “Simoni, nina neno nitakalo kukuambia.” Akasema, “Mwalimu, nena.” Akasema, “Mtu mmoja mkopeshaji alikuwa na wadeni wawili; mmoja amwia dinari mia tano, na wa pili hamsini. Nao walipokuwa hawana cha kumlipa, aliwasamehe wote wawili. Katika hao wawili ni yupi atakayempenda zaidi?” Simoni akajibu akasema, “Nadhani ni yule ambaye alimsamehe nyingi.” Akamwambia, “Umeamua haki.” Akamgeukia yule mwanamke, akamwambia Simoni, “Wamwona mwanamke huyu? Niliingia nyumbani kwako, hukunipa maji kwa miguu yangu; bali huyu amenidondoshea machozi miguu yangu; na kuipangusa kwa nywele za kichwa chake. Wewe hukunibusu; lakini huyu tangu nilipoingia hakuacha kunibusu sana miguu yangu. Hukunipaka kichwa changu mafuta; bali huyu amenipaka miguu yangu marhamu. Kwa ajili ya hayo nakuambia, Amesamehewa dhambi zake ambazo ni nyingi, kwa kuwa amependa sana; lakini asamehewaye kidogo, huyo hupenda kidogo.” Kisha alimwambia mwanamke, Umesamehewa dhambi zako.” Ndipo wale walioketi chakulani pamoja naye walianza kusema mioyoni mwao, “Ni nani huyu hata asamehe dhambi?” Akamwambia yule mwanamke, “Imani yako imekuokoa, enenda zako kwa amani.

TAFAKARI

MSAMAHA UPONYA: Mwanamke aliyempaka Yesu marhamu alifahamika na watu wengi wa eneo lile kwa sababu alikuwa na tabia ya ukahaba. Hebu jaribu kufikiria juu ya mwanamke huyu alipokuwa katika maisha yake, ni nini labda kilimfanya awe kahaba? Chupa ya marimari iliyojaa marhamu ilikuwa ghali sana. Fikiria sababu mbalimbali kwa nini achukue fedha aliyokuwa ameiweka akiba akanunua chupa ya marimari, kwa ajili ya kumpaka Kristo? Kwa nini huyu mwanamke alitaka kukutana na Yesu kwa hali ya namna hiyo akilia. Bila shaka roho ya kufanya toba ilimsukuma kukutana na Kristo katika mazingira hayo. Je unafikiri ni nini kilitokea kwanza hasa katika hali ya huyu mwanamke? Nguvu ya wongofu inatenda kazi. Katika Injili Yesu anatoa mfano wa mkopeshaji, dinarii mia tano ni sawa na mshahara wa mwaka mmoja na nusu. Dinari hamsini ni sawa na mshahara wa mwezi mmoja. Katika somo hili Yesu anatufundisha mtu aliyetenda dhambi nyingi na chache wote husamehewa, tunaposamehewa dhambi zetu tumpende na kumshukuru Mungu zaidi. 

SALA: Ee Bwana Yesu utujalie majuto kamili kwa ajili ya dhambi zetu.

About mzigotv

Nyimbo Mpya 2023, 2022 Download Audio, Video, Mp3, Mp3 African music, Tanzania Music, Naijamusic, naijavibe, Bekaboy, Djmwanga, Tanzania songs, Kenya songs, Uganda songs, Rwanda songs, Congo songs, Zanzibar, Singeli, Taarabu, Reggae, Amapiano, Nyimbo za dini, Gospel songs, Diamond platnumz, jux, Rayvanny, Harmonize, Nandy, Zuchu, Wasafi, Alikiba Teading songs, Top 100 songs youtube, Nigeria, Naija songs.

Recommended for you