Mzigo-TV-728x90

Masomo ya misa

Masomo ya Misa Mei 23

By

on

Tumsifu Yesu Kristo. Karibu Katika Masomo ya Misa 23/05/2024

2024 MEI 23 : ALHAMISI-JUMA LA 7 LA MWAKA

Mt. Desideri wa Vienne, Askofu na Mfiadini
Rangi: Kijani
Zaburi: Juma

Somo 1. Yak 5: 1-6

Haya basi, enyi matajiri! Lieni, mkapige yowe kwa sababu ya mashaka yenu yanayowajia. Mali zenu zimeoza, na mavazi yenu yameliwa na nondo. Dhahabu yenu na fedha yenu zimeingia kutu, na kutu yake itawashuhudia, nayo itakula miili yenu kama moto. Mmejiwekea akiba katika siku za mwisho. Angalieni, ujira wa wakulima waliovuna mashamba yenu, ninyi mliouzuia kwa hila, unapiga kelele, na vilio vyao waliovuna vimeingia masikioni mwa Bwana wa majeshi. Mmefanya anasa katika dunia, na kujifurahisha kwa tamaa; mmejilisha mioyo yenu kama siku ya machinjo. Mmehukumu mwenye haki mkamwua; wala hashindani nanyi.

Wimbo wa Katikati. Zab 49: 14-15

1. Hiyo ndiyo njia yao, ujinga wao,
nao walioko baada yao huyaridhia maneno yao.
Kama kondoo wamewekwa kwenda kuzimu,
Na mauti itawachunga;
Watu wanyofu watawamiliki asubuhi.

(K)Heri walio maskini wa roho, maana ufalme wa mbinguni ni wao.

2. Umbo lao linachakaa, kao lao ni kuzimu.
Bali Mungu atanikomboa nafsi yangu,
Atanitoa mkononi mwa kuzimu,
Maana atanikaribisha. (K)

3. Usiogope mtu atakapopata utajiri,
Na fahari ya nyumba yake itakapozidi.
Maana atakapokufa hatachukua chochote;
Utukufu wake hautashuka ukimfuata. (K)

4. Ajapojibariki nafsi yake alipokuwa hai,
Na watu watakusifu ukijitendea mema,
Atakwenda kwenye kizazi cha baba zake;
Hawataona nuru hata milele. (K)

Injili. Mk 9:41-50

Yesu aliwaambia wanafunzi wake: Ye yote atakayewanywesha ninyi kikombe cha maji, kwa kuwa ninyi ni watu wa Kristo, amin, nawaambia, hatakosa thawabu yake. Na ye yote atakayemkosesha mmojawapo wa wadogo hawa waniaminio, afadhali afungiwe jiwe la kusagia shingoni mwake, na kutupwa baharini. Na mkono wako ukikukosesha, ukate; ni afadhali kuingia katika uzima u kigutu, kuliko kuwa na mikono miwili, na kwenda zako jehanum, kwenye moto usiozimika; ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki. Na mguu wako ukikukosesha, ukate; ni afadhali kuingia katika uzima, u kiwete, kuliko kuwa na miguu miwili, na kutupwa katika jehanum; ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki. Na jicho lako likikukosesha, ling’oe, ulitupe; ni afadhali kuingia katika ufalme wa Mungu, una chongo, kuliko kuwa na  macho mawili, na kutupwa katika jehanum; ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki. Kwa sababu kila mtu atatiwa chumvi kwa moto. Chumvi ni njema; lakini chumvi ikiwa si chumvi tena, mtaitia nini ikolee? Mwe na chumvi ndani yenu, mkakae kwa amani ninyi kwa ninyi.

 

TAFAKARI

TUSHINDE VISHAWISHI NA VILEMA VYETU: Injili ya leo inatufundisha kuwa ndani mwetu sote kuna vitu ambavyo vinaweza kuwa vizingiti au vizuizi katika kuishi ujumbe wa Habari Njema. Tunaalikwa leo kufahamu vizuizi hivi na kuviondoa. Yesu anaposema mkono au mguu ukikukosesha uukate au jicho likikukosesha ling’oe hamaanishi kutoa viungo hivi. Badala yake Yesu anatoa tahadhari tu kuondokana na mambo yale yanayokinzana na maisha yetu ya ufuasi. Yawezekana ni kilema fulani kama vile wivu, hasira, uchoyo, uvivu, masengenyo, tamaa mbaya na mambo mengine yasiyofaa. Hivi vyote ni vitu tunavyopaswa kuvikataa ili visiwe kizuizi kwetu. Yesu anatufundisha kuwa ukarimu unalipa kwani anayetoa msaada hata mdogo tu kwa ajili ya wahitaji hawatapungukiwa. Yesu anajali sadaka na majitoleo yetu mbalimbali tunayofanya kwa lengo la kuwezesha kazi yake. Hivyo tusichoke kujitoa kwa kazi za kanisa, tusichoke kulipa zaka, tusichoke kutenda mema.

SALA: Ee Yesu utupe neema ya kushinda vilema vyetu vya kiroho.

About mzigotv

Nyimbo Mpya 2023, 2022 Download Audio, Video, Mp3, Mp3 African music, Tanzania Music, Naijamusic, naijavibe, Bekaboy, Djmwanga, Tanzania songs, Kenya songs, Uganda songs, Rwanda songs, Congo songs, Zanzibar, Singeli, Taarabu, Reggae, Amapiano, Nyimbo za dini, Gospel songs, Diamond platnumz, jux, Rayvanny, Harmonize, Nandy, Zuchu, Wasafi, Alikiba Teading songs, Top 100 songs youtube, Nigeria, Naija songs.

Recommended for you