Mzigo-TV-728x90

Masomo ya misa

Masomo ya Misa Jumamosi ya Pasaka

By

on

Tumsifu Yesu Kristo. Karibu Katika Masomo ya Misa 06/04/2024

2024 APRILI 6 : JUMAMOSO-JUMA LA KWANZA LA PASAKA                                                                                   Mt. Prudensi, Askofu
Rangi: Nyeupe
Zaburi: Tazama sala ya siku

Somo 1. Mdo 4:13-21

Siku ile, makuhani na akida wa hekalu walipoona ujasiri wa Petro na Yohane, na kuwajua ya kuwa ni watu wasio na elimu, wasio na maarifa, wakastaajabu, wakawatambua ya kwamba walikuwa pamoja na Yesu. Na wakimwona yule aliyeponywa akisimama pamoja nao hawakuwa na neno la kujibu. Wakawaamuru kutoka katika baraza, wakafanya shauri wao kwa wao, wakisema, tuwafanyieni watu hawa? Maana ni dhahiri kwa watu wote wakaao Yerusalemu ya kwamba ishara mashuhuri imefanywa nao, wala hatuwezi kuikana. Lakini neno hili lisije likaenea katika watu, na tuwatishe wasiseme tena na mtu awaye yote kwa jina hili. Wakawaita, wakawaamuru wasiseme kabisa wala kufundisha kwa jina la Yesu. Petro na Yohane wakawajibu wakawaambia, kwamba ni haki mbele za Mungu kuwasikiliza ninyi kuliko Mungu, hukumuni ninyi wenyewe; maana sisi hatuwezi kuacha kuyanena mambo tuliyoyaona na kuyasikia. Nao walipokwisha kuwatisha tena wakawafungua, wasione njia ya kuwaadhibu, kwa sababu ya watu; kwa kuwa watu wote walikuwa wakimtukuza Mungu kwa hayo yaliyotendeka.

Wimbo wa Katikati. Zab 118:1, 14-21

“1. Aleluya.
Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema,
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
Bwana ni nguvu zangu na wimbo wangu,
Naye amekuwa wokovu wangu.
Sauti ya furaha na wokovu,
Imo hemani mwao wenye haki. (K)

“Jiwe walilolikataa waashi,
Limekuwa jiwe kuu la pembeni. “

2. Mkono wa kuume wa Bwana hutenda makuu.
Mkono wa kuume wa Bwana umetukuzwa;
Mkono wa kuume wa Bwana hutenda makuu.
Sitakufa bali nitaishi,
Nami nitayasimulia matendo ya Bwana.
Bwana ameniadhibu sana,
Lakini hakuniacha nife. (K)

3. Nifungulieni malango ya haki,
Nitaingia na kumshukuru Bwana.
Lango hili ni la Bwana,
Wenye haki ndio watakaoliingia.
Nitakushukuru kwa maana umenijibu,
Nawe umekuwa wokovu wangu. (K)”

Injili. Mk 16:9-15

Yesu alipofufuka alfajiri siku ya kwanza ya juma, alimtokea kwanza Mariamu Magdalene, ambaye kwamba alimtoa pepo saba. Huyo akashika njia akawapasha habari wale waliokuwa pamoja naye, nao wakali wanaomboleza na kulia. Walakini hao waliposikia kama yu hai, naye amemwona, hawakusadiki. Baada ya hayo akawatokea watu wawili miongoni mwao, ana sura nyingine; nao walikuwa wakishika njia kwenda shamba. Na hao wakaenda zao wakawapa habari wale wengine; wala hao hawakuwasadiki. Baadaye akaonekana na wale kumi na mmoja walipokuwa wakila, akawakemea kwa kutokuamini kwao na ugumu wa mioyo yao, kwa kuwa hawakuwasadiki wale waliomwona alipofufuka katika wafu. Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.

TAFAKARI

UJASIRI WA KITUME: Tumesikia katika Injili Yesu anawaamuru mitume “Enendeni ulimwenguni mwote mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.” Huu ndio utume msingi wa Kanisa. Mtakatifu Yohani Henry Newmann anasema “Mwenyezi Mungu aliniumba kwa makusudi maalum, ana utume maalumu ambao anataka niutekeleze ambao hakuna mwingine anayeweza kuutekeleza pasipo mimi.” Hapa tuelewe kila mmoja anao utume wake, na Yesu anatutaka tutimize utume huo kwa ujasiri bila woga. Tuwe kama Petro na Yohani katika somo la kwanza, waliwajibu Makuhani na Maakida kwa ujasiri kuwa watamtii Mungu na sio wanadamu. Kama kuna kitu kimelifanya Kanisa Katoliki kuendelea kusimama imara, ni utii, utii kwa sauti ya Mungu na utii kwa uongozi halali wa Kanisa. Kama hakuna utii katika utume, basi mambo hayawezi kwenda inavyopaswa.

SALA: Ee Mungu, katika kutimiza majukumu yetu, tunaomba neema zako.

About mzigotv

Nyimbo Mpya 2023, 2022 Download Audio, Video, Mp3, Mp3 African music, Tanzania Music, Naijamusic, naijavibe, Bekaboy, Djmwanga, Tanzania songs, Kenya songs, Uganda songs, Rwanda songs, Congo songs, Zanzibar, Singeli, Taarabu, Reggae, Amapiano, Nyimbo za dini, Gospel songs, Diamond platnumz, jux, Rayvanny, Harmonize, Nandy, Zuchu, Wasafi, Alikiba Teading songs, Top 100 songs youtube, Nigeria, Naija songs.

Recommended for you