Mzigo-TV-728x90

Masomo ya misa

Masomo ya Misa Aprili 9

By

on

Tumsifu Yesu Kristo. Karibu Katika Masomo ya Misa 09/04/2024

2024 APRILI 9 : JUMANNE-JUMA LA PILI LA PASAKA

Mt. Waldetrudis
Rangi: Nyeupe
Zaburi: Juma 2

Somo 1. Mdo 4:32-37

Jamii ya watu walioamini walikuwa na moyo mmoja na roho moja; wala hapana mmoja aliyesema ya kuwa kitu cho chote alicho nacho ni mali yake mwenyewe; bali walikuwa na vitu vyote shirika. Na mitume wakatoa ushuhuda wa kufufuka kwake Yesu kwa nguvu nyingi, na neema nyingi ikawa juu yao wote. Wala hapakuwa na mtu mmoja miongoni mwao mwenye mahitaji; kwa sababu watu wote waliokuwa na viwanja au nyumba waliviuza, wakaileta thamani ya vitu vile vilivyouzwa, wakaiweka miguuni pa mitume; kila mtu akagawiwa kwa kadiri ya alivyohitaji. Na Yusufu, aliyeitwa na mitume Barnaba, (maana yake, Mwana wa faraja), Mlawi, asili yake ni mtu wa Kipro, alikuwa na shamba akaliuza, akaileta fedha, akaiweka miguuni pa mitume.

Wimbo wa Katikati. Zab 93:1-2, 5

“1. Bwana ametamalaki, amejivika adhama,
Bwana amejivika, na kujikaza nguvu. (K)

K) Bwana ametamalakai, amejivika adhama.

2. Naam, ulimwengu umethibitika usitikisike;
Kiti chako kimekuwa thabiti tokea zamani;
Wewe ndiwe uliye tangu milele. (K)

3. Shuhuda zako ni amini sana;
Utakatifu ndio uifaao nyumba yako.
Ee Bwana, milele na milele. (K)”

Injili. Yn 3:7-15

Yesu alimwambia Nikodemo: Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamna budi kuzaliwa mara ya pili. Upepo huvuma upendako, na sauti yake waisikia, lakini hujui unakotoka wala unakokwenda; kadhalika na hali yake kila mtu aliyezaliwa kwa Roho. Nikodemo akajibu, akamwambia, Yawezaje kuwa mambo haya? Yesu akajibu, akamwambia, Je, wewe u mwalimu wa Israeli, na mambo haya huyafahamu? Amin, amin, nakuambia kwamba, Lile tulijualo twalinena, na lile tuliloliona twalishuhudia; wala ushuhuda wetu hamwukubali. Ikiwa nimewaambia mambo ya duniani, wala hamsadiki, mtasadiki wapi niwaambiapo mambo ya mbinguni? Wala hakuna mtu aliyepaa mbinguni, ila yeye aliyeshuka kutoka mbinguni, yaani, Mwana wa Adamu. Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa; ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika yeye.

TAFAKARI

IMANI HUKOMAZWA NA UAMINIFU: Yesu anaikomaza imani ya Nikodemu kwa kumtaka amwamini yeye aliyeshuka toka mbinguni. Wakati mwingine imani yetu inayumba kutokana na kutokuwa na msimamo, mara leo huku kesho kule, tunakuwa watu wa kubahatisha. Ndio maana Nikodemu alitaka kujiridhisha kwa kuuliza ili ajihakikishie. Kuna watu hawaulizi mambo yaweje na matokeo yake wanajikuta wamefanya sivyo. Katika somo la kwanza tumeona jinsi mitume walivyoimarisha imani ya watu kwa kuwataka washirikishane walivyo navyo, kuondoa ubinafsi na umuhimu wa maisha ya jumuiya. Mwana falsafa Plato alisema “marafiki wa kweli huwa na vitu vyote pamoja.” Roho ya ubinafsi/umimi hudumaza sana jamii. Hii huondoa roho ya majitoleo. Wapo watu wanaojilimbikizia mali hadi hawana mahali pa kuweka, anafurahi tu kuona mlundikano wa vitu hata kama havitumii. Tunasahau alichosema Mtakatifu Tereza kuwa “hata nguo tunazovaa, ni Mungu tu ametuazima ili tusitiri miili yetu.” Kuwa na mali nyingi, haisaidii kama hakuna majitoleo.

SALA: Bwana Yesu tunaomba utupe moyo wa kupenda kushirikishana yale unayotujalia.

About mzigotv

Nyimbo Mpya 2023, 2022 Download Audio, Video, Mp3, Mp3 African music, Tanzania Music, Naijamusic, naijavibe, Bekaboy, Djmwanga, Tanzania songs, Kenya songs, Uganda songs, Rwanda songs, Congo songs, Zanzibar, Singeli, Taarabu, Reggae, Amapiano, Nyimbo za dini, Gospel songs, Diamond platnumz, jux, Rayvanny, Harmonize, Nandy, Zuchu, Wasafi, Alikiba Teading songs, Top 100 songs youtube, Nigeria, Naija songs.

Recommended for you