Mzigo-TV-728x90

Masomo ya misa

Masomo ya Misa Aprili 8

By

on

Tumsifu Yesu Kristo. Karibu Katika Masomo ya Misa 08/04/2024

2024 APRILI 8 : JUMATATU-JUMA LA PILI LA PASAKA

KUPASHWA HABARI YA KUZALIWA BWANA
Rangi: Nyeupe
Zaburi: Tazama sala ya siku

Somo 1. Isa 7: 10-14

Bwana alisema na Ahazi akinena, jitakie ishara ya Bwana, Mungu wako; itake katika mahali palipo chini sana, au katika mahali palipo juu sana. Lakini Ahazi akasema, sitaitaka, wala sitamjaribu Bwana. Naye akasema, sikilizeni sasa, enyi nyumba ya Daudi; Je! ni neno dogo kwenu kuwachosha wanadamu, hata mkataka kumchosha Mungu wangu pia? Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara. Tazama, bikira atachukua mimba, atamzaa mtoto mwanamume, naye atamwita jina lake Imanueli.

Wimbo wa Katikati. Zab 40:7-8a, 8b-9, 10, 11

“1. Dhabihu na matoleo hukupendezwa nazo,
Masikio yangu umeyazibua,
Kafara na sadaka za dhambi hukuzitaka.
Ndipo niliposema, Tazama nimekuja. (K)

(K) “Tazama, nimekuja, Ee Bwana,
kuyafanya mapenzi yako. “

2. Katika gombo la chuo nimeandikiwa
Kuyafanya mapenzi yako,
Ee Mungu wangu, ndiyo furaha yangu;
Naam, sheria yako imo moyoni mwangu. (K)

3. Nimehubiri habari za haki katika kusanyiko kubwa,
Sikuizuia midomo yangu; Ee Bwana, unajua. (K)

4. Sikusitiri haki yako moyoni mwangu;
Nimetangaza uaminifu wako na wokovu wako.
Sikuficha fadhili zako wala kweli yako
Katika kusanyiko kubwa. (K)”

Somo 2. Ebr 10:4-10

Haiwezekani damu ya mafahali na mbuzi kuondoa dhambi. kwa hiyo ajapo ulimwenguni, asema, Dhabihu na toleo hukutaka, Lakini mwili uliniwekea tayari; Sadaka za kuteketezwa na sadaka za dhambi hukupendezwa nazo; Ndipo niliposema, tazama, nimekuja, (katika gombo la chuo nimeandikiwa) Niyafanye mapenzi yako, Mungu. Hapo juu asemapo, dhabihu na matoleo na sadaka za kuteketezwa na hizo za dhambi hukuzitaka, wala hukupendezwa nazo, (Zitolewazo kama ilivyoamuru torati), Ndipo aliposema, tazama, nimekuja niyafanye mapenzi yako. Aondoa la kwanza ili kusudi alisimamishe la pili. Katika mapenzi hayo tumepata utakaso, kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo mara moja tu.

Injili. Lk 1: 26-38

Mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa Galilaya, jina lake Nazareti, kwa mwanamwali bikira aliyekuwa ameposwa na mtu, jina lake Yusufu, wa mbari ya Daudi; na jina lake bikira huyo ni Mariamu Akaingia nyumbani kwake akasema, Salamu, uliyepewa neema. Bwana yu pamoja nawe. Naye akafadhaika sana kwa ajili ya maneno yake, akawaza moyoni, Salamu hii ni ya namna gani? Malaika akamwambia, Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu. Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu. Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake. Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na ufalme wake utakuwa hauna mwisho. Mariamu akamwambia malaika, Litakuwaje neno hili, maana sijui mume? Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu. Tena, tazama, jamaa yako Elizabeti naye amechukua mimba ya mtoto mwanamume katika uzee wake; na mwezi huu ni wa sita kwake yeye aliyeitwa tasa; kwa kuwa hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu. Mariamu akasema, Tazama, mimi ni mjakazi wa Bwana; na iwe kwangu kama ulivyosema. Kisha malaika akaondoka akaenda zake.

TAFAKARI

MAPENZI YA MUNGU YATIMIZWE: Tunaadhimisha Sherehe ya Kupashwa Habari ya Kuzaliwa Bwana. Ni Sherehe ya Tangazo ya kwamba Bikira Maria atakuwa Mama wa Bwana wetu Yesu Kristo. Tunaadhimisha ukamilifu wa maneno ya Mungu kwa kinywa cha nabii Isaya kwa Ahazi aliposema, “Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita jina lake Imanueli”(Isa 7:14). Utabiri huu wa Isaya ndio unapata umbo katika tangazo la malaika Gabriel kwa Bikira Maria. “Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu”(Lk 1:31). Mariamu anasalimiwa na malaika Gabriel akimwamkia “Salamu, uliyepewa neema. Bwana yu pamoja nawe”(Lk 1:28). Mariamu anajawa na hofu kwa sababu ya salamu hiyo. Ni salamu yenye ujumbe kutoka kwa Mungu mwenyewe. Malaika anamwambia Mariamu “Usiogope” (Lk 1:30). Mariamu anaijibu salamu hiyo kwa kusema “Tazama, mimi ni mjakazi wa Bwana; na iwe kwangu kama ulivyosema”(Lk 1:38). Mariamu anatufundisha kuwa watii na kutoogopa kutimiza mapenzi ya Mungu.

SALA: Ee Mama Bikira Maria utuombee fadhila ya utii kwa Mungu.

About mzigotv

Nyimbo Mpya 2023, 2022 Download Audio, Video, Mp3, Mp3 African music, Tanzania Music, Naijamusic, naijavibe, Bekaboy, Djmwanga, Tanzania songs, Kenya songs, Uganda songs, Rwanda songs, Congo songs, Zanzibar, Singeli, Taarabu, Reggae, Amapiano, Nyimbo za dini, Gospel songs, Diamond platnumz, jux, Rayvanny, Harmonize, Nandy, Zuchu, Wasafi, Alikiba Teading songs, Top 100 songs youtube, Nigeria, Naija songs.

Recommended for you