Mzigo-TV-728x90

Masomo ya misa

Masomo ya Misa Aprili 22

By

on

Tumsifu Yesu Kristo. Karibu Katika Masomo ya Misa 22/04/2024

2024 APRILI 22 : JUMATATU-JUMA LA NNE LA PASAKA

Mt. Konrad wa Parzam, Mtawa Mfransisko
Rangi: Nyeupe
Zaburi: Juma 4

Somo 1. Mdo 11:1-18

Siku zile, mitume na ndugu waliokuwako katika Uyahudi wakapata habari ya kwamba watu wa Mataifa nao wamelipokea neno la Mungu. Na Petro alipopanda kwenda Yerusalemu, wale walio wa tohara wakashindana naye, wakisema, Uliingia kwa watu wasiotahiriwa ukala nao. Petro akaanza kuwaeleza kwa taratibu, akasema, Nalikuwa katika mji wa Yafa, nikiomba, roho yangu ikazimia, nikaona maono; chombo kinashuka, kama nguo kubwa inatelemshwa kutoka mbinguni kwa pembe zake nne, kikanifikia. Nikakitazama sana, nikifikiri, nikaona wanyama wa nchi wenye miguu minne, na wanyama wa mwituni, nao watambaao, na ndege wa angani. Nikasikia na sauti ikiniambia, Ondoka; Petro, ukachinje ule. Nikasema, Hasha, Bwana, kwa maana kitu kilicho kichafu au kilicho najisi hakijaingia kabisa kinywani mwangu. Sauti ikanijibu mara ya pili kutoka mbinguni, alivyovitakasa Mungu, usivinene wewe najisi. Jambo hili likatendeka mara tatu, kisha vitu vyote vikavutwa tena juu mbinguni. Na tazama, mara hiyo watu watatu wakasimama mbele ya nyumba tuliyokuwamo waliotumwa kwangu kutoka Kaisaria. Roho akaniambia nifuatane nao, nisione tashwishi. Ndugu hawa sita nao wakaenda nami, tukaingia katika nyumba ya mtu yule; akatueleza jinsi alivyomwona malaika aliyesimama nyumbani mwake na kumwambia, tuma watu kwenda Yafa ukamwite Simoni aitwaye Petro, atakayekuambia maneno ambayo yatakuokoa, wewe na nyumba yako yote. Ikawa nilipoanza kunena, Roho Mtakatifu akawashukia kama alivyotushukia sisi mwanzo. Nikalikumbuka neno lile la Bwana, jinsi alivyosema, Yohane alibatiza kwa maji kweli, bali ninyi mtabatiza kwa Roho Mtakatifu. Basi, ikiwa Mwenyezi Mungu amewapa wao karama ile ile aliyotupa sisi tuliomwamini Bwana Yesu Kristo, mimi ni nani niweze kumpinga Mungu? Waliposikia maneno haya wakanyamaza, wakamtukuza Mungu, wakisema, Basi, Mungu amewajalia hata mataifa nao toba liletalo uzima.

Wimbo wa Katikati. Zab 42:2-3.43:3-4

“1. Kama ayala aioneavyo shauku mito ya maji,
Vivyo hivyo nafsi yangu inakuonea shauku, ee Mungu. (K)

2. Nafsi yangu inamwonea kiu Mungu, Mungu aliye hai,
Lini nitakapokuja nionekane mbele za Mungu? (K)

3. Nilitewe nuru yako na kweli yako ziniongoze,
zinifikishe kwenye mlima wako mtakatifu na hata maskani yako. (K)

4. Hivyo nitakwenda madhabahuni kwa Mungu,
kwa Mungu aliye furaha yangu na shangwe yangu;
Nitakusifu kwa kinubi, ee Mungu, Mungu wangu. (K)”

K) Nafsi yangu inamwonea kiu Mungu, Mungu aliye hai.  

K) Nafsi yangu inamwonea kiu Mungu, Mungu aliye hai.  

Injili. Yn 10: 1-10

Yesu alisema: Mimi ndimi mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo. Mtu wa mshahara, wala si mchungaji, ambaye kondoo si mali yake, humwona mbwamwitu anakuja, akawaacha kondoo na kukimbia; na mbwamwitu huwakamata na kuwatawanya. Yule hukimbia kwa kuwa ni mtu wa mshahara; wala mambo ya kondoo si kitu kwake. Mimi ndimi mchungaji mwema; nao walio wangu nawajua; nao walio wangu wanijua mimi; kama vile Baba anijuavyo, nami nimjuavyo Baba. Nami nautoa uhai wangu kwa ajili ya kondoo. Na kondoo wengine ninao, ambao si wa zizi hili; na hao nao imenipasa kuwaleta; na sauti yangu wataisikia; kisha kutakuwako kundi moja na mchungaji mmoja. Ndiposa Baba anipenda, kwa sababu nautoa uhai wangu ili niutwae tena. Hakuna mtu aniondoleaye, bali mimi nautoa mwenyewe. Nami ninao uweza wa kuutoa, ninao na uweza wa kuutwaa tena. Agizo hilo nalilipokea kwa Baba yangu.

TAFAKARI

YESU NI MCHUNGAJI WETU: Kanisa Katoliki limekabidhiwa jukumu la kuwaelekeza watu wote kumjua Mungu. Katekisimu ya Kanisa Katoliki inasema, “Sakramenti ya ubatizo ndiyo inayomwondolea mtu dhambi ya Asili pamoja na dhambi nyinginezo, kutupatia neema ya utakaso, kutuandika watoto wa Mungu na wa Kanisa.” Ni kwa sakramenti hii tunaanza safari ya kuwa kondoo na tunapaswa kuwa chini ya mchungaji wetu Yesu Kristo. Kanisa linapaswa kuelewa kuwa, lina wajibu si tu wa kuwalinda walio ndani bali hata kuwatafuta na kuwarudisha waliopotea, (walegevu). Ukiangalia mfumo tulionao sasa wa Jumuiya Ndogondogo za Kikirsto utagundua kwa urahisi sana ni wapi kuna shida katika kuiishi imani yetu. Haitoshi kusubiri mpaka mtu afe na fomu yake kujazwa kuwa ‘hastahili kufanyiwa maziko ya Kikristo’’ kutokana na namna yake alivyokuwa anaishi. Injili hii inatutaka tumrekebishe kabla na hii ni kazi yetu sote, sio suala la kusema ni kazi ya mapadre/maaskofu la hasha, kila mbatizwa anapaswa kumlinda mwenzake, kuwa mchunguji mwema kama Kristo mwenyewe.

SALA: Ee Mungu utujalie tutambue wajibu wa kuwaongoza walio walegevu kiimani.

About mzigotv

Nyimbo Mpya 2023, 2022 Download Audio, Video, Mp3, Mp3 African music, Tanzania Music, Naijamusic, naijavibe, Bekaboy, Djmwanga, Tanzania songs, Kenya songs, Uganda songs, Rwanda songs, Congo songs, Zanzibar, Singeli, Taarabu, Reggae, Amapiano, Nyimbo za dini, Gospel songs, Diamond platnumz, jux, Rayvanny, Harmonize, Nandy, Zuchu, Wasafi, Alikiba Teading songs, Top 100 songs youtube, Nigeria, Naija songs.

Recommended for you