Mzigo-TV-728x90

Masomo ya misa

Masomo ya Misa Aprili 11

By

on

Tumsifu Yesu Kristo. Karibu Katika Masomo ya Misa 11/04/2024

2024 APRILI 11 : JUMATANO-JUMA LA PILI LA PASAKA

Mt. Stanislao, Askofu na Shahidi
Rangi: Nyeupe
Zaburi: Juma 2

Somo 1. Mdo 5:27-33

Walipowaleta mitume, waliwaweka katika baraza. Kuhani mkuu akawauliza, akisema, Je, Hatukuwaamuru ninyi kwa nguvu, msifundishe kwa jina hili? Nanyi, tazameni, mmeijaza Yerusalemu mafundisho yenu, na mnataka kuileta damu ya mtu yule juu yetu. Petro na mitume wakajibu, wakisema, imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu. Mungu wa baba zetu alimfufua Yesu, ambaye ninyi mlimwua mkimtundika katika mti. Mtu huyo Mungu amemtukuza kwa mkono wake wa kuume, awe Mkuu na Mwokozi, awape Waisraeli toba na msamaha wa dhambi. Na sisi tu mashahidi wa mambo haya, pamoja na Roho Mtakatifu ambaye Mungu amewapa wote wamtiio. Wao waliposikia wakachomwa mioyo yao; wakafanya shauri kuwaua.

Wimb o wa Katikati. Zab 34:2, 9, 17-20

“1. Nitamhimidi Bwana kila wakati,
Sifa zake zi kinywani mwangu daima.
Onjeni mwone ya kuwa Bwana yu mwema;
Heri mtu Yule anayemtumaini. (K)

K) Maskini aliita, Bwana akasikia.

2. Macho ya Bwana huwaelekea wenye haki,
Na masikio yake hukielekea kilio chao.
Walilia, naye Bwana akasikia,
Akawaponya na taabu zao zote. (K)

3. Bwana yu karibu nao waliovunjiaka moyo,
Na waliopondeka roho huwaokoa.
Mateso ya mwenye haki ni mengi,
Lakini Bwana humponya nayo yote. (K)

Injili. Yn 3:31-36

Yohane Mbatizaji aliwaambia wafuasi wake: Yeye ajaye kutoka juu, huyo yu juu ya yote. Yeye aliye wa dunia, asili yake ni ya dunia, naye anena mambo ya duniani. Yeye ajaye kutoka mbinguni yu juu ya yote. Yale aliyoyaona na kuyasikia ndiyo anayoyashuhudia, wala hakuna anayekubali ushuhuda wake. Yeye aliyeukubali ushuhuda wake ametia muhuri ya kwamba Mungu ni kweli. Kwa kuwa yeye aliyetumwa na Mungu huyanena maneno ya Mungu; kwa sababu hamtoi Roho kwa kipimo. Baba ampenda Mwana, naye amempa vyote mkononi mwake. Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia.

TAFAKARI

WOGA HUFIFISHA MAENDELEO: Yohani Mbatizaji alijitahidi kwa nguvu zote kumdhihirisha Kristo kwa watu, hakuwa mwoga na hili alilieleza wazi kwa wafuasi wake. Ukweli kumhusu Mungu Baba alitufunulia Kristo, huu ndio utume ambao Mama Kanisa amekabidhiwa ili kuwasaidia watu wote wafike kwenye uzima wa milele mbinguni. Kanisa linaalikwa kila mara kutokuwa na woga kwani woga humfanya mtu ashindwe kufanya yale yampasayo na mwisho wa siku kujikuta amepotea. Kitabu cha Matendo ya Mitume kimeeleza wazi kuwa hawakuwa na woga, pamoja na vitisho vingi toka kwa wale waliokuwa wanapingana na utume wa Kristo, bado walisimama imara na kuonesha wazi kumtii Mungu zaidi. Kuna watu wanaoonesha utii sana kwa wakuu wao wa kazi wakiogopa kufukuzwa kazi lakini hawana hofu ya Mungu. Huko ni kujisahau, wanasahau kuwa Mungu ndiye astahiliye kuogopwa na kuheshimiwa.

SALA: Ee Yesu utupe moyo wa ujasiri wa kukushuhudia kwa watu.

About mzigotv

Nyimbo Mpya 2023, 2022 Download Audio, Video, Mp3, Mp3 African music, Tanzania Music, Naijamusic, naijavibe, Bekaboy, Djmwanga, Tanzania songs, Kenya songs, Uganda songs, Rwanda songs, Congo songs, Zanzibar, Singeli, Taarabu, Reggae, Amapiano, Nyimbo za dini, Gospel songs, Diamond platnumz, jux, Rayvanny, Harmonize, Nandy, Zuchu, Wasafi, Alikiba Teading songs, Top 100 songs youtube, Nigeria, Naija songs.

Recommended for you