Mzigo-TV-728x90

Masomo ya misa

Maomo ya Misa Aprili 20

By

on

Tumsifu Yesu Kristo. Karibu Katika Masomo ya Misa 20/04/2024

2024 APRILI 20 : JUMAMOSI-JUMA LA TATU LA PASAKA

Mt. Marselino wa Embrun, Askofu
Rangi: Nyeupe
Zaburi: Juma 3

Somo 1. Mdo 9:31-42

Kanisa lilipata raha katika Uyahudi wote na Galilaya na Samaria, likajengwa, likiendelea na kuongezeka katika kicho cha Bwana, na faraja ya Roho Mtakatifu. Hata Petro alipokuwa akizunguka-zunguka pande zote akawatelemkia na watakatifu waliokaa Lida. Akamwona mtu mmoja huko, jina lake Ainea, mtu huyo amelala kitandani miaka minane; maana alikuwa amepooza. Petro akamwambia, Ainea, Yesu Kristo akuponya; ondoka, ujitandikie. Mara akaondoka. Na watu waliokaa Lida na Sharani wakamwona, wakamgeukia Bwana. Na mwanafunzi mmoja alikuwako Yafa, jina lake Tabitha, tafsiri yake ni Dorkasi (yaani paa); mwanamke huyu alikuwa amejaa matendo mema na sadaka alizozitoa. Ikawa siku zile akaugua, akafa; hata walipokwisha kumwosha, wakamweka orofani. Na kwa kuwa mji wa Lida ulikuwa karibu na Yafa, nao wanafunzi wamesikia ya kwamba Petro yuko huko, wakatuma watu wawili kwake, kumsihi na kusema, Usikawie kuja kwetu. Petro akaondoka akafuatana nao. Alipofika, wakampeleka juu orofani wajane wote wakasimama karibu naye, wakilia na kumwonesha zile kanzu na nguo alizozishona Dorkasi wakati ule alipokuwa pamoja nao. Petro akawatoa nje wote, akapiga magoti, akaomba, kisha akaelekea yule maiti, akanena, Tabitha, ondoka. Naye akafumbua macho yake na alipomwona Petro akajiinua, akaketi. Akampa mkono, akamwinua, hata akiisha kuwaita wale watakatifu na wajane akamweka mbele yao, hali yu hai. Ikajulikana katika mji mzima wa Yafa; watu wengi wakamwamini Bwana.

Wimbo wa Katikati. Zab 116:12-17

“1. Nimrudishie Bwana nini
Kwa ukarimu wake wote alionitendea?
Nitakipokea kikombe cha wokovu;
Na kulitangaza jina la Bwana. (K)

2. Nitaziondoa nadhiri zangu kwa Bwana,
Naam, mbele ya watu wake wote.
Ina thamani machoni pa Bwana
Mauti ya wacha Mungu wake. (K)

3. Ee Bwana, hakika mimi ni mtumishi wako,
Mtumishi wako, mwana na mjakazi wako,
Umenifungua vifungo vyangu.
Nitakutolea dhabihu ya kushukuru;
Na kulitangaza jina la Bwana. (K)”

K) Nimrudishie Bwana nini kwa ukarimu wake wote alionitendea?

Injili. Yn 6:60-69​

Siku ile, watu wengi miongoni mwa wanafunzi wake waliposikia maneno ya Yesu juu ya mkate wa uzima, walisema: Neno hili ni gumu, ni nani awezaye kulisikia? Naye Yesu akafahamu nafsini mwake ya kuwa wanafunzi wake wanalinung’unikia neno hilo, akawaambia, Je, neno hili linawakwaza? Itakuwaje basi, mmwonapo Mwana wa Adamu akipaa huko alikokuwako kwanza? Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima. Lakini kuna wengine miongoni mwenu wasioamini. Kwa maana Yesu alijua tangu mwanzo ni nani wasioamini, naye ni nani atakayemsaliti. Akasema, Kwa sababu hiyo nimewaambia ya kwamba hakuna mtu awezaye kuja kwangu isipokuwa amejaliwa na Baba yangu. Kwa ajili ya hayo wengi miongoni mwa wanafunzi wake wakarejea nyuma, wasiandamane naye tena. Basi Yesu akawaambia wale Thenashara, Je! ninyi nanyi mwataka kuondoka? Basi Simoni Petro akamjibu, Bwana! Twende kwa nani? Wewe unayo maneno ya uzima wa milele. Nasi tumesadiki, tena tumejua, ya kuwa wewe ndiwe Mtakatifu wa Mungu.

TAFAKARI

KWA YESU KUNA UZIMA: Kukiri kwa Petro kama tulivyosikia katika Injili “Bwana twende kwa nani? Wewe unayo maneno ya uzima wa milele” ni kielelezo tosha kuwa Kristo ni mweza wa yote, kutangatanga kwetu huku na kule kutafuta usalama hakutusaidii kitu. Hata hivyo ili kumfuata Yesu kikamilifu hatuna budi kuyaacha malimwengu (rej. Mt 19:16-22) na kuwajali wahitaji. Tukiishi hivi tunakamilika na kuishi maisha matakatifu. Ndilo hili Petro alifanya, kuwajali wahitaji: alimponya Aimea na alimfufua Dorkasi, kwa kuyafanya haya alifanya watu wengi wakamwongokea Mungu. Utume unaofanywa na Kanisa ni wa kujisadaka hasa kwa ajili ya wengine. Yesu aliwahoji wale Thenashara, “Je ninyi nanyi mwataka kuondoka?” Nasi leo tunaulizwa swali hili hili, ‘Je tunataka kuondoka? tunataka kuhama toka Katoliki na kwenda dini/madhehebu mengine?’ Perto anatusaidia kutambua kwamba kwa Yesu kuna mzima. Hivyo tumsadiki (Yesu) na kumfuata ili atufanye watakatifu.

SALA: Ee Yesu utusaidie tutambue kwamba kwako kuna uzima wetu.

About mzigotv

Nyimbo Mpya 2023, 2022 Download Audio, Video, Mp3, Mp3 African music, Tanzania Music, Naijamusic, naijavibe, Bekaboy, Djmwanga, Tanzania songs, Kenya songs, Uganda songs, Rwanda songs, Congo songs, Zanzibar, Singeli, Taarabu, Reggae, Amapiano, Nyimbo za dini, Gospel songs, Diamond platnumz, jux, Rayvanny, Harmonize, Nandy, Zuchu, Wasafi, Alikiba Teading songs, Top 100 songs youtube, Nigeria, Naija songs.

Recommended for you