Tumsifu Yesu Kristo. Karibu Katika Masomo ya Misa 24/10/2024
2024 OKTOBA 24: ALHAMISI: JUMA LA 29 LA MWAKA
Mt. Antoni Maria Klaret, Askofu
Rangi: Nyeupe
Zaburi: Juma I
SOMO 1. Efe 3:14-21
Nampigia Baba magoti, ambaye kwa jina lake ubaba wote wa mbinguni na wa duniani unaitwa, awajalieni, kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake, kufanywa imara kwa nguvu, kwa kazi ya Roho wake, katika utu wa ndani. Kristo akae mioyoni mwenu kwa imani mkiwa na shina na msingi katika upendo; ili mpate kufahamu pamoja na watakatifu wote jinsi ulivyo upana, na urefu, na kimo na kina; na kuujua upendo wake Kristo, upitao ufahamu kwa jinsi ulivyo mwingi, mpate kutimilika kwa utimilifu wote wa Mungu. Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu; naam, atukuzwe katika Kanisa na katika Kristo Yesu hata vizazi vyote vya milele na milele. Amina. |
WIMBO WA KATIKATI. Zab 33:1-2, 4-5, 11-12, 18-19
1. Mpigieni Bwana vigelegele, enyi wenye haki, (K) Nchi imejaa fadhili za Bwana. 2. Kwa kuwa neno la Bwana lina adili, 3. Shauri la Bwana lasimama milele, 4. Tazama, la Bwana li kwao wamchao, |
INJILI. Lk 12:49-53
Yesu aliwaambia wanafunzi wake: “Nimekuja kutupa moto duniani; na ukiwa umekwisha washwa, ni nini nitakalo zaidi? Lakini nina ubatizo unipasao kubatiziwa, nami nina dhiki kama nini hata utimizwe! Je! Mwadhani ya kwamba nimekuja kuleta amani duniani? Nawaambia, La, sivyo, bali mafarakano. kwa kuwa tokea sasa katika nyumba moja watakuwamo watu watano wamefarakana, watatu kwa wawili, wawili kwa watatu. Watafarakana baba na mwanawe, na mwana na babaye; mama na binti yake, na binti na mamaye; mkwe mtu na mkwewe, mkwe na mkwe mtu.” |
TAFAKARI
UAMINIFU KATIKA FAMILIA: “Nawaambia, La, sivyo, bali mafarakano. kwa kuwa tokea sasa katika nyumba moja watakuwamo watu watano wamefarakana,” Kuna wakati familia zinaweza kupanga mipango ya siri na serikali au na watu fulani kumuangamiza/ kuwaangamiza ndugu zao. Katika nchi ambazo walau ukristo unavumilika, familia zinaweza kuchukizwa sana na kitendo cha mwanafamilia kuongoka. Hili linaweza kupelekea kuwatenga na kuwafukuza na hata kuwanyima urithi. Katika mambo hayo yote Yesu anabaki kuwa ni Bwana, na uhusiano mwingine wa aina yoyote unapaswa kuchukua nafasi ya pili. Katika sehemu nyingi hapa ulimwenguni, kumekuwa na changamoto nyingi katika kumfuta Kristo, lakini pamoja na changamoto hizo, tunapaswa kuachana na yale yote yanayofungamana na familia kwa ajili ya Kristo. Je! upo tayari kuipoteza familia yako, kuwapoteza marafiki wa karibu? Je! upo tayari kukataliwa na kuuawa kwa ajili ya Kristo? SALA: Ee Mungu utujalie kukupatia wewe nafasi ya kwanza katika maisha licha ya vipingamizi tunavyokutana navyo katika familia na ndugu zetu. |
The post Masomo ya Misa Oktoba 24 appeared first on CLARETIAN PUBLICATIONS-EAST AFRICA.