Masomo ya misa

Masomo ya Misa Novemba 8

By

on

Tumsifu Yesu Kristo. Karibu Katika Masomo ya Misa 08/11/2024

2024 NOVEMBA 8: IJUMAA: JUMA LA 30 LA MWAKA

Mt. Godfrei wa Amiens, Askofu
Rangi: Kijani

Zaburi: Juna III

SOMO 1. Flp 3: 17 – 4: 1

Ndugu zangu, mnifuate mimi, mkawatazame wao waendao kwa kuufuata mfano tuliowapa ninyi. Maana wengi huenenda, ambao nimewaambieni mara nyingi habari zao, na sasa nawambia hata kwa machozi, kuwa ni adui za msalaba wa Kristo; Mwisho wao ni uharibifu, mungu wao ni tumbo, utukufu wao u katika fedheha yao, waniao mambo ya dunia. Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia mwokozi, Bwana Yesu Kristo; atakayeubadili mwili wetu wa unyonge, upate kufanana na mwili wake wa utukufu, kwa uweza ule ambao kwa huo aweza hata kuvitiisha vitu vyote viwe chini yake. Basi ndugu zangu, wapendwa wangu, ninaowaonea shauku, furaha yangu, na taji yangu, hivyo simameni imara katika Bwana, wapenzi wangu. 

WIMBO WA KATIKATI. Zab 122: 1-5

1. Nalifahamu waliponiambia, 
Na twende nyumbani kwa Bwana.
Miguu yetu imesimama
Ndani ya malango yako, Ee Yerusalemu.

(K) Nalifurahi waliponiambia, na twende nyumbani kwa Bwana.

2. Ee Yerusalemu uliyejengwa
Kama mji ulioshikamana,
Huko ndiko walikopanda kabila,
Kabila za Bwana. (K)

3. Ushuhuda kwa Israeli,
Walishukuru jina la Bwana.
Maana huko viliwekwa viti vya hukumu,
Viti vya enzi vya mbari ya Daudi. (K)

INJILI. Lk 16:1-8

Yesu aliwaambia wanafunzi wake: Palikuwa na mtu mmoja, tajiri, aliyekuwa na wakili wake; huyu alishitakiwa kwake kuwa anatapanya mali zake. Akamwita, akamwambia, Ni habari gani hii ninayosikia juu yako? Toa hesabu ya uwakili wako, kwa kuwa huwezi kuwa wakili tena. Yule wakili akasema moyoni mwake, Nifanyeje? Maana, bwana wangu ananiondolea uwakili. Kulima, siwezi; kuomba, naona haya. Najua nitakalotenda, ili nitakapotolewa katika uwakili, wanikaribishe nyumbani mwao. Akawaita wadeni wa bwana wake, kila mmoja; akamwambia wa kwanza, Wawiwani na bwana wangu? Akasema, Vipimo mia vya mafuta. Akamwambia, Twaa hati yako, keti upesi, andika hamsini. Kisha akamwambia mwingine, Na wewe wawiwani? Akasema, Makanda mia ya ngano. Akamwambia, Twaa hati yako, andika themanini. Yule bwana akamsifu wakili dhalimu kwa vile alivyotenda kwa busara; kwa kuwa wana wa ulimwengu huu katika kizazi chao wenyewe huwa na busara kuliko wana wa nuru.

NGUVU YA PESA NA MUDA: Pesa inaleta kishawishi cha kutaka ubwana. Tumia rasilimali ulizonazo kwa busara kwa sababu ni mali ya Bwana na sio yako. Pesa inaweza ikatumika kwa mambo mabaya au kwa mambo mema. Pesa ina nguvu kubwa kwa hiyo unapaswa kuitumia kwa uangalifu na busara. Tumia rasilimali zako katika namna ile itakayoamsha imani na utii kwa Mungu. Katika Maandiko Matakatifu, wakili alitumia muda na fursa aliyokuwa nayo. Usikubali muda uishe kabla hujafanya mambo ya muhimu katika maisha. Tumia fursa alizokupatia Mungu. Pengine ulifanya kazi hadi usiku wakati familia yako bado changa na sasa umejikusanyia na unakila kitu na watoto wako ni watu wazima sasa. Labda ulitaka kumwambia mama au baba yako jinsi walivyo wa muhimu na unavyowapenda lakini amefariki kabla hata hujasema. Pengine ulitaka kuungana tena na Mungu na kuziungama dhambi zako, labda ulitaka kuanza kumwabudu Mungu baada ya muda mrefu wa kumwacha, wakati ndio huu.

SALA: Bwana unijalie kila siku kutumia vyema muda unaonipatia.

 

The post Masomo ya Misa Novemba 8 appeared first on CLARETIAN PUBLICATIONS-EAST AFRICA.

About mzigotv

Nyimbo Mpya 2025 2024 2023 2022 Download Audio, Video, Mp3, Mp3 African music, Tanzania Music, Naijamusic, naijavibe, Bekaboy, Djmwanga, Tanzania songs, Kenya songs, Uganda songs, Rwanda songs, Congo songs, Zanzibar, Singeli, Taarabu, Reggae, Amapiano, Nyimbo za dini, Gospel songs, Diamond platnumz, jux, Rayvanny, Harmonize, Nandy, Zuchu, Wasafi, Alikiba Teading songs, Top 100 songs youtube, Nigeria, Naija songs.

Recommended for you