Masomo ya misa

Masomo ya Misa: Novemba 16

By

on

Jumamosi Juma la 32
Kumbukumbu
Rangi: Kijani
Zaburi: Juma 4

Mt. Margareta, Malkia Wa Skotland (1046-1093)

Utume: Aliolewa na mfalme wa Skotland, Malkolm wa Tatu. Margareta aliweza kumwongoza malkoni, kuilainisha tabia yake ngumu, na kumfanya awe mwenye fadhila nyingi, upendo wa kidugu, haki na huruma. Fadhila kuu ya malkia huyo ilikuwa upendo wake kwa maskini.

SOMO 1: 3 Yoh 1:5-8

Mpenzi, kazi ile ni ya uaminifu uwatendeayo hao ndugu na hao wageni nao, waliokushuhudia upendo wako mbele ya kanisa; utafanya vizuri ukiwasafirisha kama ipasavyo kwa Mungu. Kwa maana, kwa ajili ya Jina hilo, walitoka, wasipokee kitu kwa Mataifa. Basi imetupasa sisi kuwakaribisha watu kama hao, ili tuwe watenda kazi pamoja na kweli.

WIMBO WA KATIKATI: Zab 112:1-6

“1. Aleluya.
Heri mtu yule amchae Bwana,
Apendezwaye sana na maagizo yake
Wazao wake watakuwa Hodari duniani;
Kizazi cha wenye adili kitabarikiwa.

(K) Heri mtu yule amchaye Bwana.

  1. Nyumbani mwake mna utajiri na mali,
    Na haki yake yakaa milele.
    Huru huwazukia wenye adili gizani;
    Ana afadhali na huruma na haki. (K)
  2. Heri atendaye Fadhili na kukopesha;
    Atengenezaye mambo yake kwa haki.
    Kwa maana hataondoshwa kamwe;
    Mwenye haki atakumbukwa milele. (K)”

INJILI: Lk 18:1-8

Yesu aliwaambia wanafunzi wake mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu siku zote, wala wasikate tamaa. Akasema, Palikuwa na kadhi katika mji fulani, hamchi Mungu, wala hajali watu. Na katika mji huo palikuwa na mwanamke mjane, aliyekuwa akimwendea-endea, akisema, Nipatie haki na adui wangu. Naye kwa muda alikataa; halafu akasema moyoni mwake, Ijapokuwa simchi Mungu wala sijali watu, lakini, kwa kuwa mjane huyu ananiudhi, nitampatia haki yake, asije akanichosha kwa kunijia daima. Bwana akasema, Sikilizeni asemavyo yule kadhi dhalimu. Na Mungu, je! Hatawapatia haki wateule wake wanaomlilia mchana na usiku, naye ni mvumilivu kwao? Nawaambia, atawapatia haki upesi; walakini, atakapokuja Mwana wa Adamu, je! Ataiona imani duniani?

TAFAKARI

SALINI SANA: Yesu aliwafundisha wafuasi wake wadumu katika sala. Mtu mmoja alikuwa amevaa koti limeandikwa “Sali sana.” Mtu anasalije sana? Tusiangalie sala kama mtu anavyofanya kazi. Lakini kusali sana kunahusisha mambo matatu; Imani, Matumaini na Mapendo. Imani: Wale wasioamini wanaweza wakawa wanasumbuliwa na hasira, chuki au kukata tamaa pale wanapokumbana na matatizo. Lakini kwako wewe unayeamini, Mungu analo suluhisho kwa ajili yako. Sala inajenga imani. Matumaini: Maisha yanaisha, wakati mwingine mwisho wake unakua mbaya au mzuri lakini kwa vyovyote vile maisha yanafika mwisho wake. Mungu ametupatia ahadi ya uzima wa milele kwa wale wanaomtumainia. Kila unaposali unaamsha upya matumaini yako kwa maisha yajayo pamoja na Mungu. Kudumu katika sala kunazaa matumaini. Upendo: kujifikiria nafsi yako mwenyewe, matendo na matatizo yako, ni jambo la kawaida. Kuwajali wengine kunapingana na hisia za kujipenda mwenyewe. Mungu anatutaka tujifunze kupenda na kuwaonesha wengine upendo. Kumbuka sala inakuza upendo.

SALA: Nikiongozwa na Imani, Matumaini na Mapendo Ee Bwana unijalie kudumu katika sala.

About mzigotv

Nyimbo Mpya 2025 2024 2023 2022 Download Audio, Video, Mp3, Mp3 African music, Tanzania Music, Naijamusic, naijavibe, Bekaboy, Djmwanga, Tanzania songs, Kenya songs, Uganda songs, Rwanda songs, Congo songs, Zanzibar, Singeli, Taarabu, Reggae, Amapiano, Nyimbo za dini, Gospel songs, Diamond platnumz, jux, Rayvanny, Harmonize, Nandy, Zuchu, Wasafi, Alikiba Teading songs, Top 100 songs youtube, Nigeria, Naija songs.

Recommended for you