Mzigo-TV-728x90

Masomo ya misa

Masomo ya Misa Juni 26

By

on

Tumsifu Yesu Kristo. Karibu Katika Masomo ya Misa 26/06/2024

2024 JUNI 26: JUMATANO; JUMA  12 LA MWAKA

Mt. Antelmi, Askofu
Rangi: 
Zaburi:

Somo 1. 2 Fal 22:8-13; 23:1-3

Hilkia, kuhani mkuu, alimwambia Shafani, mwandishi, nimekiona kitabu cha torati katika nyumba ya Bwana. Hilkia akampa Shafani kile kitabu, naye akakisoma. Shafani mwandishi akamwendea mfalme, akamletea mfalme habari tena, akasema, Watumishi wako wamezitoa zile fedha zilizoonekana ndani ya nyumba, nao wamewakabidhi wafanyakazi wanaosimamia nyumba ya Bwana. Kisha Shafani mwandishi akamwambia mfalme, akasema, Hilkia kuhani amenipa kitabu. Shafani akakisoma mbele ya mfalme. Ikawa, mfalme alipokwisha kuyasikia maneno ya kitabu hicho cha torati, alirarua nguo zake. Mfalme akamwamuru Hilkia kuhani, na Ahikamu, mwana wa Shafani, na Akbori, mwana wa Mikaya, na Shafani mwandishi, na Asaya, mtumishi wa mfalme, akasema, Enendeni, mkamwulize Bwana kwa ajili yangu, na kwa ajili ya watu hawa, na kwa ajili ya Yuda yote, katika habari za maneno ya kitabu hiki kilichoonekana; kwa kuwa hasira ya Bwana ni kubwa aliyotukasirikia, kwa sababu baba zetu hawakuyaangalia maneno ya kitabu hiki, kufanya kama hayo yote tuliyoandikiwa. Kisha, mfalme akatuma wajumbe, nao wakamkusanyia wazee wote wa Yuda na wa Yerusalemu. Mfalme akapanda kwenda nyumbani kwa Bwana, na watu wote wa Yuda, nao wote waliokaa Yerusalemu, pamoja naye, na makuhani, na manabii, na watu wote, wadogo kwa wakubwa; akasoma masikioni mwao maneno yote ya kitabu cha agano kilichoonekana katika nyumba ya Bwana. Mfalme akasimama karibu na nguzo, akafanya agano mbele za Bwana, kumfuata Bwana, na kuyashika maagizo yake, na shuhuda zake, na amri zake, kwa moyo wake wote, na kwa roho yake yote, na kuyathibitisha maneno ya agano hilo yaliyoandikwa katika kitabu hicho; nao watu wote wakalikubali agano lile.

Wimbo wa Katikati. Zab 119:33-37, 40

1. Ee Bwana, unifundishe njia ya amri zako,
Nami nitaishika hata mwisho.
Unifahamishe nami nitaishika sheria yako,
Naam, nitaitii kwa moyo wangu wote.

(K) Ee Bwana, unifundishe njia ya amri zako.

2. Uniendeshe katika mapito ya maagizo yako,
Kwa maana nimependezwa nayo.
Unielekeze moyo wangu na shuhuda zako,
Wala usiielekee tamaa. (K)

3. Unigeuze macho yangu nisitazame visivyofaa,
Unihuishe katika njia yako.
Tazama, nimeyatamani mausia yako,
Unihuishe kwa haki yako. (K)

Injili. Mt 7:15-20

Yesu aliwaambia wanafunzi wake: Jihadharini na manabii wa uwongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali.  Mtawatambua kwa matunda yao.  Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti?  Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya. Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri. Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni.  Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua.

TAFAKARI

MANENO YETU YAENDANE NA MATENDO YETU: Wakati wa Yesu walikuwepo manabii wa uongo waliowahubiria watu ujumbe tofauti na ule wa Yesu. Katika Injili ya leo Yesu anatupa tahadhari juu ya manabii wa namna hii. Katika jamii zetu nyakati hizi wapo manabii wengi kabisa wa uongo hivyo tusiwafungulie milango hata kidogo, kwani hawana nia njema na imani yetu. Wapo wanaohubiri dhihaka dhidi ya imani yetu, wapo wanaotumia mwavuli wa Ukristo ili kujinufaisha wenyewe, wapo wanaotoa tafsiri potofu ya baadhi ya vifungu vya Neno la Mungu ili kukidhi matakwa yao, wapo wanaodai kupata ufunuo au kuoteshwa na Mungu. Hawa tusiwape nafasi wala kuwasikiliza kwani wana umahiri katika kuongea na kuwaahidi watu mafanikio ya haraka sana na hivyo ni hatari kwa imani yetu. Katika kutambua roho ya unabii wa uongo Yesu anatupa nyenzo za kutumia na nyenzo hizo ni kutazama matendo yao. Matendo ya manabii wa uongo hayaendani na maneno yao. Hivyo tujikite katika imani yetu na tusikubali kuyumbishwa na manabii wanaotafuta maslahi binafsi. 

SALA: Ee Yesu nijaalie neema ili niyaweka maneno (imani) yangu katika maatendo mema.

About mzigotv

Nyimbo Mpya 2023, 2022 Download Audio, Video, Mp3, Mp3 African music, Tanzania Music, Naijamusic, naijavibe, Bekaboy, Djmwanga, Tanzania songs, Kenya songs, Uganda songs, Rwanda songs, Congo songs, Zanzibar, Singeli, Taarabu, Reggae, Amapiano, Nyimbo za dini, Gospel songs, Diamond platnumz, jux, Rayvanny, Harmonize, Nandy, Zuchu, Wasafi, Alikiba Teading songs, Top 100 songs youtube, Nigeria, Naija songs.

Recommended for you