Masomo ya misa

Masomo ya Misa: Disemba 4

By

on

Jumatano: Juma la I la Majilio
Kumbukumbu ya hiyari
Rangi: Kijani
Zaburi: Juma I

SOMO 1. Isa 25:6-10

Siku ile Bwana wa majeshi atawafanyia mataifa yote karamu ya vitu vinono, karamu ya divai iliyokaa juu ya urojorojo wake, karamu ya vinono vilivyojaa mafuta, karamu ya divai iliyokaa juu ya urojorojo wake, iliyochujwa sana. Naye katika mlima huu atauharibu uso wa sitara iliyowekwa juu ya watu wote, na utaji ule uliotandwa juu ya mataifa yote. Amemeza mauti hata milele; na Bwana Mungu atafuta machozi katika nyuso zote; na aibu ya watu wake ataiondoa katika ulimwengu wote; maana Bwana amenena hayo. Katika siku hiyo watasema, Tazama, huyu ndiye Mungu wetu, ndiye tuliyemngoja atusaidie; huyu ndiye Bwana tuliyemngoja, na tushangilie na kuufurahia wokovu wake.  Kwa maana mkono wa Bwana utatulia katika mlima huu.

WIMBO WA KATIKATI. Zab 23:1-3, 4-6

1. Bwana ndiye mchungaji wangu,
Sitapungukiwa na kitu.
Katika malisho ya majani mabichi hunilaza,

(K) Nitakaa nyumbani mwa Bwana milele.

2. Kando ya maji ya utulivu huniongoza,
            Hunihuisha nafsi yangu na kuniongoza.
            Katika njia za haki kwa ajili ya jina lake. (K)

3. Waandaa meza mbele yangu,
            Machoni pa watesi wangu.
            Umenipaka mafuta kichwani pangu,
            Na kikombe changu kinafurika. (K)

4. Hakika wema na fadhili zitanifuata
Siku zote za maisha yangu;
Nami nitakaa nyumbani mwa Bwana milele. (K)

INJILI. Mt 15:29-37

Siku ile: Yesu, alifika kando ya bahari ya Galilaya; akapanda mlimani, akaketi huko. Wakamwendea makutano mengi wakimletea viwete, vipofu, mabubu, vilema, na wengine wengi, wakawaweka miguuni pake; akawaponya; hata ule mkutano wakastaajabu, walipowaona mabubu wanasema, vilema wanakuwa wazima, viwete wanakwenda, na vipofu wanaona; wakamtukuza Mungu wa Israeli.  Yesu akawaita wanafunzi wake, akasema, Nawahurumia mkutano, kwa kuwa yapata siku tatu wamekaa pamoja nami, wala hawana kitu cha kula; tena kuwaaga wakifunga sipendi, wasije wakazimia njiani. Wanafunzi wake wakamwambia, Tupate wapi mikate mingi hapa nyikani, hata kushibisha mkutano mkuu namna hii? Yesu akawaambia, Mnayo mikate mingapi? Wakasema, Saba, na visamaki vichache.  Akawaagiza mkutano waketi chini; akaitwaa ile mikate saba na vile visamaki, akashukuru akavimega, akawapa wanafunzi wake, nao wanafunzi wakawapa makutano. Wakala wote wakashiba; wakayaokota masazo ya vipande vya mikate, makanda saba, yamejaa.

TAFAKARI

UPONYAJI: Umati mkubwa ulikuja kwa Yesu ili awaponye. Hata sasa Yesu bado anaponya mioyo iliyovunjika, na tunaweza kuwaleta kwake wale wote wanaoteseka. Ni nani unadhani anahitaji uponyaji kutoka kwa Yesu? Walete watu hao kwa Yesu kwa njia ya sala, au kwa kuwaeleza sababu za kuwa na matumaini kama uliyonayo wewe. (rej. 1Pet 3:15). Kisha umwache Kristo awaponye. Wayahudi walimshukuru Mungu kabla na baada ya kula chakula. Watu wengi wanaona kusali kabla na baada ya kula ni jambo lililopitwa na wakati. Lakini Yesu kamwe hakuacha kumshukuru Mungu Baba yake. Kumshukuru Mungu kabla ya kula kunatukumbusha kwamba, chakula, kushiba, furaha katika chakula na hata maisha yenyewe vimetoka kwa Mungu. Kama uliacha kusali wakati wa chakula anza sasa. Kama imekuwa ni tabia yako kusali kabla na baada ya kula, endelea na tabia hiyo ukiwa na shukrani.

SALA: Ee Mungu utujalie sikuzote kukumbuka kuwaleta kwako katika sala wale walio katika changamoto mbali mbali, na hasa waliokata tamaa. 

About mzigotv

Nyimbo Mpya 2025 2024 2023 2022 Download Audio, Video, Mp3, Mp3 African music, Tanzania Music, Naijamusic, naijavibe, Bekaboy, Djmwanga, Tanzania songs, Kenya songs, Uganda songs, Rwanda songs, Congo songs, Zanzibar, Singeli, Taarabu, Reggae, Amapiano, Nyimbo za dini, Gospel songs, Diamond platnumz, jux, Rayvanny, Harmonize, Nandy, Zuchu, Wasafi, Alikiba Teading songs, Top 100 songs youtube, Nigeria, Naija songs.

Recommended for you