Tumsifu Yesu Kristo. Karibu Katika Masomo ya Misa 26/05/2024
2024 MEI 20 : JUMAPILI-UTATU MTAKATIFU
Rangi: Nyeupe
Zaburi: Tazama sala ya Siku
Somo 1. Kum 4:32-34, 39-40
Musa aliwaambia makutano: Uliza sasa siku zilizopita, zilizokuwa kabla yako, tangu siku ile Mungu aliyoumba mwanadamu juu ya nchi, na toka pembe hii ya Mbingu hata pembe hii, kwamba kumetukia neno lolote kama hili kubwa, au kwamba kumesikiwa habari ya neno kama hili? je! watu wakati wowote wamesikia sauti ya Mungu ikinena toka kati ya moto, kama wewe ulivyosikia, wasife? Au Mungu amekwenda wakati gani akajitwalia taifa toka kati ya taifa lingine, kwa majaribu, na kwa ishara, na kwa maajabu, na kwa vita, na kwa mkono hodari, na kwa mkono ulionyoshwa, na kwa maogofya makuu, kama vile Bwana, Mungu wenu, alivyowatendea ninyi katika Misri, mbele ya macho yenu? Kwa hiyo ujue, leo hivi ukaweke moyoni mwako, ya kuwa Bwana ndiye Mungu katika mbingu juu, na katika nchi chini; hapana mwingine. Basi, zishike sheria zake, na amri zake, ninazokuamuru leo, upate kufanikiwa, wewe na watoto wako baada yako, na siku zako ziwe nyingi katika nchi ile akupayo Bwana, Mungu wako, milele. |
WIMMBO WA KATIKATI. Zab 33:4-6, 9, 18-20, 22
1. Kwa kuwa neno la Bwana ni adili, (K)Heri taifa ambalo Bwana ni Mungu wao. Na jeshi lake lote kwa pumzi ya kinywa chake. 3. Tazama, jicho la Bwana li kwao wamchao, 4. Nafsi zenu zinamngoja Bwana, |
Somo 2. Rum 8:14-17
Kila mtu anayeongozwa na Roho wa Mungu, Huyo ndiye mtoto wa Mungu. Kwa kuwa hamkupokea tena Roho ya utumwa iletayo hofu; Bali mlipokea Roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, aba, yaani, baba. Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu; na kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithi pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye. |
Injili. Mt 28:16-20
Wale wanafunzi kumi na mmoja wakaenda Galilaya, mpaaka mlima ule aliowaagiza Yesu. Nao walipomwona, walimsujudia; lakini baadhi yao waliona shaka. Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote Mbinguni na Duniani. Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza, kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu, na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari. |
TAFAKARI
TUMEUMBWA KATIKA SURA NA MFANO WA UTATU MTAKATIFU SALA: Ee Mungu utuzidishie imani juu ya Fumbo lako la Utatu Mtakatifu. |