Mzigo-TV-728x90

Masomo ya misa

Masomo ya Misa Juni 4

By

on

Tumsifu Yesu Kristo. Karibu Katika Masomo ya Misa 04/06/2024

2024 JUNI 4 : JUMANNE-JUMA LA 9 LA MWAKA

Mt. Fransisko Karachololi
Rangi: Nyekundu
Zaburi: Juma 4

Somo 1. 2 Pet 3:11-15, 17-18

Ndugu wapendwa, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa, mkitazamia hata ije siku ile ya Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu zitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka? Lakini, kama ilivyo ahadi yake, tunatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yake. Kwa hiyo, wapenzi, kwa kuwa mnatazamia mambo hayo, fanyeni bidii ili muonekane katika amani kuwa hamna mawaa wala aibu mbele yake. Nanyi uhesabuni uvumilivu wa Bwana wetu kuwa ni wokovu, kama vile na ndugu yetu mpenzi Paulo alivyowaandikia kwa hekima aliyopewa.  Basi, wapenzi mkitangulia kujua hayo, jilindeni nafsi zenu, msije mkachukuliwa na kosa la hao wahalifu, mkaanguka na kuuacha uthibitifu wenu. Lakini, kueni katika neema, na katika kumjua Bwana wetu na Mkombozi Yesu Kristo. Utukufu una yeye sasa na hata milele. Amina.

Wimbo wa Katikati. Zab 90:2-4, 10, 14, 16

1. Kabla haijazaliwa milima, wala hujaiumba dunia,
Na tangu milele hata milele ndiwe Mungu.

(K)Wewe Bwana, umekuwa makao yetu, kizazi baada ya kizazi.

2. Wamrudisha mtu mavumbini,
Usemapo, Rudini, enyi wanadamu.
Maana miaka elfu machoni pako
Ni kama siku ya jana ikiisha kupita,
Na kama kesha la usiku. (K)

3. Siku za miaka yetu ni miaka sabini,
Na ikiwa tuna nguvu miaka themanini;
Na kiburi chake ni taabu na ubatili,
Maana chapita upesi tutatokomea mara. (K)

4. Utushibishe asubuhi kwa Fadhili zako,
Nasi tutashangilia na kufurahia siku zetu zote
Matendo yako na yaonekane kwa watumishi wako,
Na adhama yako kwa Watoto wao. (K)

Injili. Mk 12:13-17

Walituma kwa Yesu baadhi ya Mafarisayo na Maherodi, ili wamnase kwa maneno. Hata walipofika walimwambia, “Mwalimu, twajua ya kuwa wewe u mtu wa kweli, wala hujali cheo cha mtu; kwa maana hutazami sura za watu; lakini katika kweli waifundisha njia ya Mungu.  Je! Ni halali kumpa Kaisari kodi au siyo? Tumpe, tusimpe?” Naye, akijua unafiki wao, akawaambia, “Mbona mmenijaribu?  Nileteeni dinari niione.” Wakaileta.  Akawaambia, “Ni ya nani sanamu hii na anwani hii?” Wakamwambia, “Ni ya Kaisari.” Yesu akajibu, akawaambia, Mpeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na yaliyo ya Mungu mpeni Mungu.” Wakamstaajabia sana.

TAFAKARI

WAJIBU WETU KWA MUNGU NA KWA JAMII: Katika Liturujia ya Neno leo kwenye Injili tumesikia Yesu akiulizwa swali la mtego ili aingizwe hatiani. Suala la kodi liliigawa sana jamii kwa wakati ule. Endapo Yesu angejibu kuwa ni sawa kulipa kodi kwa Kaisari baadhi ya wafuasi wake wangekwazika na endapo angesema si sawa kulipa kodi kwa Kaisari angekuwa kinyume na mamlaka ya kiserikali. Jibu la Yesu “Ya Kaisari mpeni Kaisari na ya Mungu mpeni Mungu” linatufundisha kutekeleza wajibu wetu kwa Mungu na kwa jamii pasipo kisingizio. Wajibu wetu kwa Mungu ni kumjua, kupenda na kumtumikia kwa kushika vema amri zake. Wajibu wetu wa kulipa kodi kwa mamlaka husika unapaswa kupewa kipaumbele. Ni vizuri mamlaka husika zitoe elimu sahihi kuhusu ulipaji wa kodi na faida zake kama uboreshwaji wa miundombinu mbalimbali ili walipakodi washawishike kulipa kodi bila hila. Pia mamlaka za kodi wawe na mfumo rafiki wa kutoza kodi bila kuwabugudhi walipaji.

Sala: Ee Yesu utujalie neema ya kutimiza majukumu yetu kwa Mungu na kwa jamii.

About mzigotv

Nyimbo Mpya 2023, 2022 Download Audio, Video, Mp3, Mp3 African music, Tanzania Music, Naijamusic, naijavibe, Bekaboy, Djmwanga, Tanzania songs, Kenya songs, Uganda songs, Rwanda songs, Congo songs, Zanzibar, Singeli, Taarabu, Reggae, Amapiano, Nyimbo za dini, Gospel songs, Diamond platnumz, jux, Rayvanny, Harmonize, Nandy, Zuchu, Wasafi, Alikiba Teading songs, Top 100 songs youtube, Nigeria, Naija songs.

Recommended for you