Nyimbo Mpya

Litania ya Mama Bikira Maria

By

on

Litania ya Mama Bikira Maria

Bwana utuhurumie.

Bwana utuhurumie.

Kristo utuhurumie.

Kristo utuhurumie.

Bwana utuhurumie.

Bwana utuhurumie.

Kristo utusikie.

Kristo utusikilize

Baba wa mbinguni, Mungu, utuhurumie.

Mwana Mkombozi wa dunia, Mungu, utuhurumie.

Roho Mtakatifu, Mungu, utuhurumie.

Utatu Mtakatifu, Mungu mmoja, utuhurumie.

Kiitikio: Utuombee

Maria Mtakatifu,

Mzazi Mtakatifu wa Mungu,

Bikira Mtakatifu, Mkuu wa mabikira,

Mama wa Kristu,

Mama wa neema ya Mungu,

Mama mtakatifu sana,

Mama mwenye usafi wa moyo,

Mama usiye na doa,

Mama usiye na dhambi,

Mama mpendelevu,

Mama mstaajabivu,

Mama wa shauri jema,

Mama wa Mwumba,

Mama wa Mkombozi,

Bikira mwenye utaratibu,

Bikira mwenye heshima,

Bikira mwenye sifa,

Bikira mwenye enzi,

Bikira mwenye huruma,

Bikira amini,

Kikao cha haki,

Kikao cha hekima,

Sababu ya furaha yetu,

Chombo cha neema,

Chombo cha heshima,

Chombo bora cha ibada,

Waridi lenye fumbo,

Mnara wa Daudi,

Mnara wa pembe,

Nyumba ya dhahabu,

Sanduku la Agano,

Mlango wa mbingu,

Nyota ya asubuhi,

Afya ya wagonjwa,

Makimbilio ya wakosefu,

Mfariji wa wenye uchungu,

Msaada wa Wakristu,

Malkia wa Malaika,

Malkia wa Mababu,

Malkia wa Manabii,

Malkia wa Mitume,

Malkia wa Mashaidi,

Malkia wa Waungama,

Malkia wa Mabikira,

Malkia wa Watakatifu wote,

Malkia uliyeumbwa, pasipo dhambi ya asili,

Malkia uliyepalizwa mbinguni,

Malkia wa Rozari takatifu,

Malkia wa amani.

Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za ulimwengu, utusamehe, Bwana.

Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za Ulimwengu, utusikilize, Bwana.

Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za ulimwengu, utuhurumie.

K. Utuombee, Mzazi Mtakatifu wa Mungu.

W. Tujaliwe ahadi za Kristu.

About admin