upload

Music News

Nililipa Tsh Milioni 500 ili nitoke Wasafi – Harmonize

on


Msanii Rajabu Abdul  maarufu Harmonize (27)  amesema aliuza nyumba zake tatu na baadhi ya mali ili kuilipa lebo ya Wasafi Sh milioni 500 kwa ajili ya kupata  hakimiliki ya kutumia nyimbo zake na jina.

Webp.net-gifmaker-549e78a6857f911ce.gif

Harmonize ameeleza hayo  katika kipindi cha moja ya redio hapa nchini

Amebainisha kuwa mkataba alioingia na lebo ya Wasafi inayomilikiwa na msanii Diamond Platnumz ilikuwa na kipengele cha kulipa kiasi hicho cha fedha ikiwa atavunja mkataba ili aweze kuendelea kutumia nyimbo pamoja na jina lake la kisanii.

“Mkataba ulinitaka nilipe Sh500 milioni na gharama za kuandaa nyimbo zangu zote wakati nikiwa chini ya Wasafi,” amesema Harmonize.

Amebainisha kuwa alifanikiwa kulipa kiasi kikubwa cha fedha hizo  jambo lililomuwezesha kuendelea kutumia nyimbo zake na jina.

Akizungumzia uhusiano wake na lebo ya Wasafi, Harmonize amesema si mzuri kama zamani, “licha ya kuwa niliondoka baada ya kupata baraka zote kutoka kwa uongozi wa Wasafi.”

Amefafanua kuwa kulikuwa na tatizo ambalo walishindwa kulimaliza alipokuwa katika lebo hiyo na aliamua kujitoa.

“Bado naamini mimi ni familia ya Wasafi na ninawaheshimu sana. Nilitoka si kwa ubaya na wala ugomvi. Nilikaa na uongozi na kuomba ridhaa yao nifanye muziki wangu mwenyewe baada ya kuona tumeshindwa kumaliza mambo yetu,” amesema.

About Mr. Frank

Mr Frank is the Founder and CEO of Mzigotv Media Group. He is a Professional blogger, Wordpress designer, Developer and Innovator on digital ideas around the world. He is skilled for more than ten years. Vision of mzigotv.com is to connect Music industry and fans in the same room easily.

Recommended for you

1 Comment