Habari

Wizara ya Afya Yatoa Taarifa Kuhusu Ugonjwa Uliozua Taaruki Bukoba

By

on

Enjoy Free Music, Audio, Video, Tanzania Music, Kenya, Uganda, Rwanda, Ghana, Nigeria here at Number One Music Platform in Tanzania

Serikali kupitia Wizara ya Afya imetoa tahadhari juu ya uwepo wa ugonjwa ambao bado haujajulikana Mkoani Kagera katika Wilaya ya Bukoba Vijijini ambapo Watu 7 wanasadikika walipata dalili za homa, kutapika, kutokwa damu maeneo mbalimbali ya mwili na figo kushindwa kufanya kazi na Watu watano kati yao wamefariki na wengine wawili wako Hospitali wanaendelea na matibabu.

Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu ametoa taarifa hiyo leo katika Ofisi za Wizara Jijini Dodoma “Wizara imepokea taarifa za uwepo wa ugonjwa ambao bado haujajulikana Kagera, Bukoba Vijijini, Kata ya Maruku na Kanyangercko, Vijiji vya Bulinda na Butayaibega, mwenendo wa ugonjwa huu unaashiria uwezekano kuwa ni ugonjwa wa kuambukiza hivyo Serikali inaendelea kufuatilia kwa karibu kuhusu mwenendo wa ugonjwa huu na kuchukua hatua za kudhibiti ili usisambae”- Prof. Tumaini Nagu
Prof. Nagu amewataka Wananchi kuwahi kituo cha kutolea huduma za afya kwa ajili ya uchunguzi na matibabu endapo ataona dalili kama kupatwa na homa, kutapika, kuharisha, kutoka damu na mwili kuishiwa nguvu, pia amewakumbusha kuwahi Kutoa taarifa mapema kwenye kituo cha kutolea huduma kilicho karibu au kupiga simu namba 199 bila malipo endapo utamuona au kukutana na Mtu mwenye dalili kama hizo.

About mzigotv

Nyimbo Mpya 2022, Mp3 Mp4 Mzigotv, Audio, Video Mpya, Tanzania Mp3, Tanzania trending songs, Nyimbo Mpya 2022, 2021, Download Audio Mzigotv, Alikiba Mp3, Video, Dj mwanga, nyimbo mpya za wiki hii dj mwanga, Rayvanny, Harmonize, Diamond Platnumz, Alikiba, Jux, Nandy, Zuchu, Lavalava, Mbosso, Bekaboy, Yingamedia, Diamond Platnumz Songs 2022


Notice: Trying to get property of non-object in /home/tjsxvbmy/public_html/wp-content/themes/osage/functions.php on line 1056

Notice: Trying to get property of non-object in /home/tjsxvbmy/public_html/wp-content/themes/osage/functions.php on line 1060

Recommended for you