Habari

Mtoto wa Rais Museveni Atangaza nia ya Kumrithi Urais Baba yake

By

on

Mtoto wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni, Muhoozi Kainerugaba ametangaza nia ya kutaka kumrithi Baba yake kwenye kiti cha Urais wa Uganda ambapo amesema atagombea Urais wa Nchi hyo mwaka 2026.

“Katika jina la Yesu Kristo, kwa jina la Vijana wa Uganda na Dunia kwa ujumla na katika jina la Mapinduzi makubwa nitagombea Urais mwaka 2026”
“Fidel Castro Shujaa wangu alikuwa Rais akiwa na umri wa miaka 32, ninakaribia kufikia miaka 49, sio sawa kabisa (Kutokuwa Rais), Vijana wanapaswa kuwa Marais wa Mataifa yao”
“Nani anakubaliana na Mimi kwamba muda wetu Vijana umewadia?, inatosha sasa kuendelea kuongozwa na Wazee na kututawala, ni muda wa Vijana kung’aa, Waziri Mkuu wa Uingereza ana miaka 42, Waziri Mkuu wa Finland ana miaka 37, sisi wengine tunakaribia miaka 50, tumechoka kusubiri, nitasimama kugombea” amesema Muhoozi ambaye ni Mkuu wa zamani wa Jeshi la Ardhini la Uganda.

About mzigotv

Nyimbo Mpya 2022, Mp3 Mp4 Mzigotv, Audio, Video Mpya, Tanzania Mp3, Tanzania trending songs, Nyimbo Mpya 2022, 2021, Download Audio Mzigotv, Alikiba Mp3, Video, Dj mwanga, nyimbo mpya za wiki hii dj mwanga, Rayvanny, Harmonize, Diamond Platnumz, Alikiba, Jux, Nandy, Zuchu, Lavalava, Mbosso, Bekaboy, Yingamedia, Diamond Platnumz Songs 2022


Notice: Trying to get property of non-object in /home/tjsxvbmy/public_html/wp-content/themes/osage/functions.php on line 1056

Notice: Trying to get property of non-object in /home/tjsxvbmy/public_html/wp-content/themes/osage/functions.php on line 1060

Recommended for you