Habari

Fiston Mayele Awaita Mashabiki Uwanja Wa Mkapa Leo Wapate Burudani Dhidi Ya US Monastir

By

on

 

Fiston Mayele Awaita Mashabiki Uwanja Wa Mkapa Leo Wapate Burudani Dhidi Ya US Monastir

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Fiston Kalala Mayele, amesema wanachotakiwa kukifanya mashabiki wa timu hiyo ni kuhakikisha wanajaa katika Uwanja wa Mkapa, kisha suala la ushindi waliache kwao.

Kauli ya Mayele imekuja wakati leo Yanga ikiwa mwenyeji wa US Monastir, katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika Kundi D utakaochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar.

Mayele katika kikosi cha Yanga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu, amefanikiwa kufunga mabao mawili, yote akiwatungua Real Bamako, ugenini na nyumbani.

Akizungumza na Spoti Xtra, Mayele alisema kuwa: “Kinachotakiwa kufanywa na mashabiki wa Yanga ni kuhakikisha wanakuja kwa wingi uwanjani na suala la ushindi watuachie sisi wachezaji tuwafurahishe.

“Huu ni mchezo ambao utatuheshimisha sisi kwa namna moja ama nyingine jambo ambalo wachezaji wote wameapa kuitafutia ushindi timu.

“Viongozi tayari wametuahidi mambo mazuri, lakini hata sisi tunataka kuweka rekodi yetu msimu huu katika michuano ya kimataifa, hivyo tutalipambania hilo.”

Naye mshambuliaji wa Yanga, Kennedy Musonda, alisema: “Mchezo huu ni muhimu sana kwetu, hakuna kingine ambacho tunahitaji zaidi ya usindi, tunawaahidi hilo mashabiki zetu.”

STORI: MARCO MZUMBE

About mzigotv

Nyimbo Mpya 2022, Mp3 Mp4 Mzigotv, Audio, Video Mpya, Tanzania Mp3, Tanzania trending songs, Nyimbo Mpya 2022, 2021, Download Audio Mzigotv, Alikiba Mp3, Video, Dj mwanga, nyimbo mpya za wiki hii dj mwanga, Rayvanny, Harmonize, Diamond Platnumz, Alikiba, Jux, Nandy, Zuchu, Lavalava, Mbosso, Bekaboy, Yingamedia, Diamond Platnumz Songs 2022


Notice: Trying to get property of non-object in /home/tjsxvbmy/public_html/wp-content/themes/osage/functions.php on line 1056

Notice: Trying to get property of non-object in /home/tjsxvbmy/public_html/wp-content/themes/osage/functions.php on line 1060

Recommended for you