Habari
Alikiba akanusha kuepo kwenye Album ya Davido, aingia kwenye kilimo
on

Msanii Alikiba ameongea kuhusu kuwekeza kwenye kilimo cha mazao tofautitofauti ya biashara zikiwemo mbogamboga, nyanya na vitunguu ambapo amesema amechagua Mkoa wa Dodoma kwasababu kuna fursa za kilimo na anaamini atapata pesa nyingi.
Alikiba amesema pamoja na mambo mengine amevutiwa na sera za Serikali ya Rais Dkt. Samia na Waziri wa Kilimo kwa namna ambavyo wamekuwa wakitatua changamoto za Wakulima na kuwatafutia masoko.
Katika hatua nyingine Alikiba amekanusha kuwepo Kwa colabo yake na Davido kama ambavyo ilisambaa mtandaoni post ikionesha Track List ya nyimbo zitakazopatikana Kwenye Album ya Davido.
Notice: Trying to get property of non-object in /home/tjsxvbmy/public_html/wp-content/themes/osage/functions.php on line 1056
Notice: Trying to get property of non-object in /home/tjsxvbmy/public_html/wp-content/themes/osage/functions.php on line 1060